October 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Yanga kuwa vaa Kagera Sugar bila Mwamnyeto

Bakari Mwamnyeto

Spread the love

 

Klabu ya soka ya Yanga leo 29 Septemba 2021, itanza kutupa karata yake ya kwanza katika Ligi Kuu Tanzania Bara ugenini dhidi ya Kagera Sugar katika Uwanja wa  Kaitaba bila ya kuwa na nahodha wao Bakari Nondo Mwamnyeto alieye pata majeruhi mazoezi. Anaripoti Damas Ndelema TUDARCo(endelea)….. 

Mchezaji huyo ambaye pia ni nahodha wa timu hiyo amekua na kiwango kizuri kwa kutengeneza kombinesheni bora na mlinzi mwenzie wa kati Dickson Job ataukosa mchezo huu wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na majeraha aliyoyapata akiwa mazoezi  hivyo kupelekea kukosa mchezo huu

Akizungumza  kuelekea mchezo wao wa leo dhidi ya Kagera Sugar Afisa habari wa Klabu ya Yanga Hassan Bumbuli amesema kua wachezaji wengi wote wapo vizuri kuelekea mchezo huo isipokua watamkosa nahodha wao Bakari Nondo  Mwamnyeto alipata majeruhi wakati wakiwa mazoezini hivyo kupelekea kukosa mchezo huo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara 

“Kwenye mchezo wa leo tutamkosa nahodha wetu, Bakari Nondo Mwamnyeto ambaye alipata majeruhi kidogo katika siku mbili hizi za mazoezi, ila wachezaji wote waliobaki wapo vizuri na timamu kwa ajili ya mchezo huo, huku wakijua malengo ya klabu kwa msimu huu ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara”. Alisema Bumbuli

Timu hizo zitakutana huku zikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare kwa kufungana bao 3-3 katika mchezo wao wa mwisho kukutana katika Ligi Kuu msimu uliopita katika dimba la Benjamini Mkapa Stadium jijini Dar es salaam

error: Content is protected !!