May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga kumbakisha Metacha, kumpa mkataba mnono

Metacha Mnata

Spread the love

 

IKIWA msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaelekea mwishoni na klabu mbalimbali zimeanza kufanya mandalizi ya usajili, klabu ya Yanga ipo kwenye mazungumzo na mlinda mlango wake, Metacha Mnata kwa ajili ya kumpa mkataba mpya. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mnata alisaini Yanga mkataba wa miaka miwili ambao unatarajia kumalizika mwisho wa msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakafikia kikomo hivi karibuni.

MwanaHALISI Online lilimtafuta Meneja wa mchezaji huyo, Jemedari Said kufuatia taarifa ya kuwa mlinda mlango huyo tayari ameshasaini mkataba mpya na waajili wake wa sasa na kusema kuwa wapo kwenye hatua ya mazungumzo.

“Hajaongeza mkataba ila tupo kwenye mazungumzo ya kuongoza mkataba na klabu yake ya Yanga nadhani mambo yataenda vizuri,” alisema Jemedari.

Metacha ambaye amekuwa na msimu nzuri toka ajiunge na Yanga kwa kuwa kipa namba moja na kucheza michezo mingi kuliko mlinda mlango mwenzie kutoka nchini Kenya. Farouk Shikalo.

Mlinda mlango huyo alijiunga na Yanga kwenye msimu wa 2019/20 akitokea klabu ya Mbao FC iliyokuwa inashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo kwa sasa ipo ligi daraja la kwanza.

Kwenye msimu huu wa Ligi Kuu 2020/21 Metacha ameshika nafasi ya pili baada ya kucheza michezo 11 bila kuruhusu bao (Clean Sheet) akiwa na kikosi cha Yanga huku nafasi ya kwanza ikishikwa na Aishi Manula mara baada ya kucheza michezo 13 bila kuruhusu bao.

error: Content is protected !!