May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga kumalizna na Namungo, Simba bado kitendawili

Spread the love

KIKOSI cha Yanga kesho kitashuka Uwanjani kwenye mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Namungo Fc, utakaochezwa kwenye Uwanja wa Majaliwa, huku michezo yao miwili dhidi ya Simba bado ikiwa kitendawili. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Ligi hiyo kwa sasa ipo kwenye duru la 29, huku Simba na Namungo FC wakiwa hawajecheza mchezo hata mmoja katika michezo miwili licha ya kucheza michezo 25 kwa kila timu.

Kwenye ratiba ya awali ilionesha Namungo walipaswa kucheza na Simba Tarehe 19 Disemba 2020 kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza lakini haukufanikiwa kuchezwa kutokana kuwepo kwa ratiba ya michezo ya kimataifa.

Timu hizo pia zilipaswa kucheza mchezo wa mzunguko wa pili Tarehe 15 Mei 2021, uliarishwa kutokana na Simba kushuka uwanjani kwenye tarehe hiyo nchini Afrika Kusini dhidi ya Kaizer Chiefs.

Mabadiliko hayo ya ratiba kwa timu hizo mbili yamekuja kutokana na ushiriki wao kwenye michuano ya kimataifa ambapo Namungo Fc aliishia hatua ya makundi kombe la shirikisho barani Afrika, huku Simba ikiwakilisha nchi kwenye klabu bingwa na kufanikiwa kufuzu kwenye hatua ya robo fainali na kesho itashuka nyumbani ugenini dhidi ya kaizer Chiefs.

Namungo inakwenda kumalizana na Yanga kesho mara baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0, wakiwa nyumbani dhidi ya Mtibwa Sugar huku wakitoka sare ya bao 1-1, kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Yanga uliochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Yanga inaingia kwenye mchezo wa kesho ugenini ikiwa na pointi 57 kwenye nafasi ya pili mara baada ya kucheza michezo 27, nyuma ya Simba iliyokuwa kileleni ikiwa na pointi 61 na michezo 25.

Namungo mara baada ya kushinda michezo miwili mfululizo imejikita kwenye nafasi ya 10 ikiwa na pointi 35, huku ikiwa imecheza michezo 25.

error: Content is protected !!