July 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga kukabidhiwa kombe jijini Mbeya

Spread the love

 

Mara baada ya tarehe 15 Juni 2022, kutangzwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, klabu ya Yanga itakabidhiwa rasmi kombe lake kwenye mchezo wa mzunguko wa 29, dhidi ya Mbeya. Anaripoti kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo utapigwa tarehe 25 Juni, kwenye dimba la CCM Sokoine jijini Mbeya, ambapo Yanga itakuwa na kibarua kizito dhidi ya wenyeji wao, klabu ya Mbeya City.

Akliweka wazi juu ya taarifa hiyo, Afisa Habari wa Bodi ya Ligi Kareem Boimanda amesema kuwa mchezo huo utatumika kuwakabidhi Yanga kombe la sambamba na Medali.

“Bodi ya Ligi inatangaza rasmi itatumia mchezo wa mzunguko wa 29, kati ya Mbeya City dhidi ya Yanga, utatumika rasmi kukabidhi kikombe cha ubingwa kwa Yanga kama mabingwa kwa msimu huu.”

“Bodi ya Ligi inawajuza kuwa maofisa wote wameshataarifiwa juu ya jambo hili na maandalizi yanaendelea vyema.” Alisema msemaji huyo

Yanga imetwaa ubingwa huo, mara baada ya kuukosa kwa kipindi cha miaka mine na hivyo kufanya hili kuwa taji lao la 28 katika historia ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika mchezo wa kwanza ambao Yanga walishuka dimbani dhidi ya Mbeya City, kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, walitoshana nguvu kwa kwenda sare ya bila kufungana.

Yanga wanaingia kwenye mchezo huo, huku wakilinda rekodi yao ya kutopoteza mchezo wowote kwenye Ligi Kuu mpaka sasa.

error: Content is protected !!