Tuesday , 21 March 2023
Home Kitengo Michezo Yanga kujipima ubavu kwa Mlandege
Michezo

Yanga kujipima ubavu kwa Mlandege

Spread the love

TIMU Yanga kesho itacheza mchezo wa kujipima nguvu dhidi mabingwa wa Ligi Kuu visiwani Zanzibar, Mlandege katika kujiweka sawa kuwakabili Kagera Sugar kwenye mchezo ujao. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Yanga itacheza mchezo huo majira ya Saa 1 jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamanzi kabla ya kusafiri kwenda mkoani Kagera kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa siku ya Jumamosi 18 septemba, 2020 kwenye dimba la Kaitaba.

Mchezo huo ambao utakuwa na umuhimu mkubwa kwa Yanga ili kujiweka sawa kwa kuwa imefanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi chake ambacho kina wachezaji wapya zaidi ya 12.

Yanga inaingia kwenye mchezo huo, huku ikiwa imeshacheza michezo miwili kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara na kuambulia alama 4, baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City na kutoka sare na Tanzania Prisons.

Mlandege FC wao watatumia mchezo huo kujiweka sawa kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi na michuano ya kimataifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa

Spread the loveUONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais...

Michezo

Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya

Spread the loveWAKATI timu ya Simba ikiibuka na ushindi wa bao 3-0...

Michezo

Taasisi ya TKO na TFF yawapiga msasa makocha wa kike 54

Spread the love WAKATI Soka la wasichana likichipua kwa kasi Taasisi ya...

Michezo

Kimwanga CUP yazidi kutimua vumbi

Spread the loveMASHINDANO ya mpira wa miguu ya Kimwanga CUP ya kuwania...

error: Content is protected !!