May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga kujipima nguvu na African Sports

Spread the love

 

KIKOSI cha Yanga kitashuka dimbani kuikabili African Sports kwenye mchezo wa kupima nguvu utakaochezwa majira ya saa 1 usiku kwenye dimba la Azam Complex, Chamazi siku ya Jumamosi tarehe 6 Februari 2021. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… (endelea)

Yanga imeingia kambini 25 Januari 2021, kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo mchezo wao unaofuata watawakabili Mbeya City tarehe 14 Februari 2021, kwenye Uwanja wa Sokonine Mbeya.

Timu hiyo itatua mchezo huo kujiweka sawa baada ya Ligi hiyo kusimama kwa mwezi mmoja kupisha michuano ya kombe la Mapinduzi na michuano ya kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan).

Mara ya mwisho Yanga kushuka dimbani ilikuwa 13 Januari mwaka huu, kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi ambapo walifanikiwa kuifunga Simba kwenye mchezo wa Fainali kwa njia ya penati kutwaa kombe hilo.

Viingilio kwenye mchezo huo vimeshawekwa wazi ambapo kiingilio cha bei ya chini kitakuwa shilingi 3,000 kwa mzunguko, huku VIP itakuwa shilingi 5,000.

error: Content is protected !!