TIMU ya Yanga ya Dar es Salaam Tanzania, itaanza kutupa karaka yake ya kwanza kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika bila uwepo wa mashabiki. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Yanga itaanza raundi ya kwanza kesho Jumapili tarehe 12 Septemba 2021, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kuwavaa River United ya Nigeria.
Uamuzi wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho kuchezwa pasina mashabiki kwa raundi ya kwanza, umetolewa leo Jumamosi, tarehe 11 Septemba 2021 na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Taarifa ya TFF iliyotolewa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa shirikisho hilo, Cliford Mario Ndimbo imesema, wamepokea maelekezo kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuwa michezo hiyo ichezwe bila mashabiki.
Lengo ni kujikinga na maambuzi ya virusi vya ugonjwa wa corona (COVID-19).
“Tunaendelea na jitihada kuhakikisha tunakubaliana na masharti ya CAF kuhakikisha mechi zinazofuata zinaruhusiwa kuingiza watazamaji,” amesema Ndimbo.
Yanga na Simba zinawakilisha klabu bingwa ambapo Simba itaanza hatua ya pili huku Azam na Biashara zikiwakilisha Kombe la Shirikisho.
Leave a comment