December 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga kama Simba, sasa kutangaza utalii Zanzibar na kilimanjaro

Spread the love

 

KLABU ya soka ya Yanga leo imeingia makubaliano maalumu ya kutangaza vivutio vya utalii kwa viwani Zanzibar na Mlima wa Kilimanjoro kupitia michuano ya kimataifa. Anaripoti Wiston Josia, TUDARCo

Yanga ambayo hii leo imenasafiri kuelekea nchini Nigeria, kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa hatua ya awali wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Rivers United.

Katika mkutano huo uliofanyika hii leo jijini Dar es Salaamambao pia uliudhuliwa na  Waziri wa maliasili na utalii Damas Ndumbalo, Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Jaji mstaafu Thomas  Mihayo aliwapongeza klabu ya Yanga kwa kufikia hatua hiyo ya kutangaza utalii wan chi bila gharama yoyote.

Yanga itatangaza vivutio hivyo kupitia nembo itakayokaa kwenye jezi ikiwa na maneno yatakayoandikwa “Visiti Kilimanjaro and Zanziba”

Kwa upande wa Waziri wa maliasili na Utalii mh,Ndumbalo amesema kuwa klabu hiyo kukubali kutangaza utalii ni jambo la kujivunia.

“kwa klabu kubwa kama yanga kukubali kutangaza utalii ni jambo kubwa na la kujivunia tunawashukulu na kuwaombea kupata ushindi na mafanikio katika mashindano yao” alisema waziri huyo.

Yanga sasa itakuwa inaungana na Simba kwenye kutangaza utalii wan nchi kupitia jezi watakazovaa kwenye michuano ya kimataifa.

Simba na Yanga zote zinashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambao Yanga tayari imeanzia kwenye hatua ya awali na Simba itaanza kwenye mzunguko wa kwanza.

error: Content is protected !!