May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga hoi mbele ya Azam FC

Spread the love

BAO la dakika ya 86 lililofungwa na Prince Dube lilitosha kuifanya Azam FC kutoka kifua mbele kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Yanga. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo ulipigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam majira ya saa 2:15 usiku.

Katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo timu zote zilishambuliana kwa zamu licha ya kumaliza dakika 45 za kwanza bila bao lolote.

Kipindi cha pili kililejea na makocha wa pande zote mbili wakajaribu kufanya mabadiliko kwa upande wa Azam FC walimtoa Yahaya Zaidi na kuingia Never Tigere, Yanga wao wakampumzisha Michael Sarpong na nafasi yake kuchukuliwa na Feisal Salumu.

Kwenye dakika ya 86 Price Dube alifanikiwa kuipatia Azam FC bao kwa shuti kali lililodumu mpaka dakika 90 za mchezo.

Kwa matokeo hayo Yanga inaendelea kusalia kwenye nafasi ya pili wakiwa na pointi 57, alama moja nyuma ya Simba wenye pointi 58 wakiwa kileleni kwenye msimamo.

Azam FC wanaendelea kubaki kwenye nafasi ya tatu wakiwa na pointi 54.

Mchezo ujao Yanga wataivaa Simba tarehe 8 Mei 2021 kwenye dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

error: Content is protected !!