June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga hiyooooo, yanusa ubingwa

Wachezaji wa Yanga wakishangilia moja kati ya mabao yao mbele ya mashabiki wao uwanja wa Taifa

Spread the love

YANGA sasa haikamatiki. Klabu Yanga imezidi kuonyesha kuwa sasa hakuna timu inatakayoikwamisha katika mbio zake ya ubingwa msimu huu wa 2014/15, baada ya leo jioni kuongeza pointi tatu muhimu baada ya kuifumua Mbeya City mabao 3-1. Anaripoti Erasto Stanslaus … (endelea).

Kwa ushindi huo uliopata katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Yanga imezidi kujikita kileleni baada ya kufikiwa pointi 46 na kuwaacha Azam FC kwa tofauti ya pointi nane wakiwa katika nafasi ya pili.

Mahasimu wa Yanga, Simba wao wapo katika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 35, hivyo nao wanaingia katika mbio za kusaka nafasi ya pili, huku dua zao zikiwa kwa Azam ifanye vibaya nao washinde michezo yao iliyobaki.

Mabao ya Yanga katika mchezo huo yalifungwa na Kpah Sherman dakika ya 20, Salum Telela dakika ya 36 na bao la tatu lilifungwana Nadir Haroub ‘Cannavaro’ dakika ya 49. Bao la Mbeya City limefungwa na Them Felix dakika ya 42.

Mbeya walilazimika kumaliza mchezo huo wakiwa pungufu baada ya mchezaji wao Them kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Telela.

error: Content is protected !!