August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga hawajaacha kitu, yatwaa mataji yote msimu huu

Spread the love

MARA Baada hii leo tarehe 2 Julai 2022, klabu ya soka ya Yanga kufanikiwa kutwaa taji la kombe la Shirikisho la Azam, timu hiyo imeweka rekodi ya kufanikiwa kutwaa matji yote nadni ya msimu huu 2021/22. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa vuta ni kuvute ulipigwa majira ya saa 9:00 kwenye dimba la Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.

Hili ni taji la tatu kwa Yanga kwa msimu huu, mara baada ya siku chache hapo nyuma kukabidhiwa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara, mara baada ya kukaa katika kipindi cha miaka mine bila kulibeba.

Licha ya taji hilo la Ligi Kuu, Yanga pia kwa msimu huu wamefanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii kwa kumfunga wapinzani wao wa karibu klabu ya Simba kwa bao 1-0.

Katika dakika 120 za mchezo wa leo timu hizo zote mbili zilitoka sare ya mabao 3-3, na kulazimika fainali hiyo kuamuliwa kwa changamoto ya mikwaju ya Penati.

Kwenye mikwaju hiyo ya Penati Yanga walifanikiwa kufunga penati zote nne walizopiga wachezaji wake Dikson Job, Yanick Bangala, Heritie Makambo na Khalid Aucho.

Kwa upande wa Coastal Union wao walikosa mikwaju miwli ya penati na kupata mmoja, ambao ulifungwa na kiungo wao fundi Victor Akpan.

Mabao ya Coastal Union kwenye mchezo wa leo, yote yaliwekwa kambani na Abdul Seleman Sopu, kwenye dakika za 10, 88, 98.

Huku mabao ya Yanga yakifungwa na Feisal Salum dakika ya 57, Makambo dakika ya 82 na Denis Nkane kwenye dakika ya 113.

Mara ya mwisho kwa Yanga kutwaa mataji hayo matatu ilikuwa kwenye msimu wa 2016/17, timu hiyo ikiwa chini ya kocha Hans Pluijm.

error: Content is protected !!