Tuesday , 21 March 2023
Home Kitengo Michezo Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa
Michezo

Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

UONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan zimeongeza ari kubwa kwa wachezaji kuipigania timu yao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yamesemwa na Mratibu wa Yanga, Hafidh Salehe, wakati wa uchezeshaji wa droo ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam hatua ya robo fainali, iliyofanyika jana katika ofisi za Azam Media.

Salehe alisema kipindi cha nyuma timu yao ilikuwa inaishia hatua ya awali ya michuano ya Kimataifa, lakini sasa vijana wamekuwa na hamasa kubwa ya kuipigania nembo ya timu yao.

“Sisi kwa sasa tunashukuru kwa hamasa hii, unawaona kabisa wachezaji wanavyopambana ili kuipatia timu matokeo mazuri uwanjani, hivyo tunashukuru kwa kila kitu kinachochangia ushindi wetu.

“Historia imebadilika na wakati huu tunaenda kwenye mechi ya mwisho wa wiki tukiwa na shauku kubwa ya kuona timu yetu inashinda mbele ya wageni wetu US Monastir, mchezo utakaopigwa siku ya Jumapili katika Uwanja wa Taifa wa Benjamini Mkapa, jijini Dar es Salaam,” alisema.

Yanga na Simba wanaogelea bahari ya fedha za Rais Samia aliyeahidi kununua kwa Sh Milioni 5, kila goli linalopatikana kwa timu hizo katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya

Spread the loveWAKATI timu ya Simba ikiibuka na ushindi wa bao 3-0...

Michezo

Taasisi ya TKO na TFF yawapiga msasa makocha wa kike 54

Spread the love WAKATI Soka la wasichana likichipua kwa kasi Taasisi ya...

Michezo

Kimwanga CUP yazidi kutimua vumbi

Spread the loveMASHINDANO ya mpira wa miguu ya Kimwanga CUP ya kuwania...

Michezo

Watanzania wang’ara Kilimanjaro International Marathon

Spread the loveWANARIADHA wa kitanzania wameng’ara katika mbio za 21 za Kilimanjaro...

error: Content is protected !!