August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga, Azam zatinga nusu fainali.

Spread the love

KLABU za Azam FC na Yanga zimetinga robo fainali baada ya kufanikiwa kusonga mbele nkwenye fainali za kombe la Shirikisho baada ya kupata ushindi katika Michezo yao iliyochezwa  leo ya hatua ya robo fainali. Anaandika Kelvini Mwaipungu

Azam ilicheza na Prison kutoka mbeya katika Uwanja wa Azam Complex, huku Yanga ikipambana Ndanda Mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga ilipata ushindi wa Mabao 2-1 dhidi ya Ndanda Fc mchezo ulioonekana kuwa mgumu kwa pande zote mbili. Katika Mchezo mwingine Azam FC nayo ilipata ushindi wa Mabao 3-1 dhidi ya Tanzania Prison.

Kwa upande wa  mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa Yanga ilifanikiwa kupata mabao kupitia kwa mshambuliaji wake Paul Nonga katika dakika ya 27 na lingine likifungwa na beki Kelvin Yondani .

Goli hilo lilipatikana kwa njia ya mkwaju wa penati dakika ya 69 baada ya Simoni Msuva kufanyiwa madhambi na Paul Ngalema ambaye alionyeshwa kadi ya pili ya njano iliyo zaa kadi nyekundu na bao pekee la Ndanda lilifungwa na Kigi Makasi katika dakika ya 56.

Vile vile  katika uwanja wa Azam Complex, Azam FC ilipata mabao yake kupitia kwa mlinzi wao wa pembeni Shomali Kampombe aliyefunga mabao mawili katika dakika ya 9 na 60 bao jingine lilifungwa na Hamisi Mcha dakika ya 86.

Tanzania Prison ilipata bao moja tu ambalo lilifungwa na Jeremiah dakika 31 mchezo mwingine wa Kombe la Shirikisho unatarajiwa kuchezwa mwishoni mwa juma hili.

error: Content is protected !!