September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yametimia: CUF hatarini kumeguka tena

Spread the love

VURUGU zimeibuka katika Kongamano la kuwarehemu wafuasi wa Chama cha Wananchi CUF, waliouawa katika maandamano ya Visiwani Zanzibar tarehe 26 na 27 Januari, 2001. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea)

Vurugu hizo zimeibuka baada ya wanachama kadhaa wa CUF kuvamia kongamano hilo huku wakibeba mabango yanayopinga migogoro inayoendelea ndani ya chama hicho, ikiwemo kujizulu kwa Abdul Kambaya, Aliyekuwa Mkurugenzi wa Habari, Mawasiliano na Umma CUF.

Baadhi ya wafuasi hao walipinga kujiuzulu kwa Kambaya, kwa maelezo kwamba hakutendewa haki kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa kwenye chama. Pia, alikuwa miongoni mwa wahanga wa maandamano ya Januari 26 na 27.

error: Content is protected !!