May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yacouba, Mukoko waitwa timu za Taifa

Yacouba Sogne mchezaji wa Yanga na timu ya Taifa ya Burkina faso

Spread the love

 

Kwa mara ya kwanza toka aliposajiliwa ndani ya klabu ya Yanga mshambuliaji kutoka Burkina Faso Yacouba Sogne ameitwa kwenye timu yake ya Taifa kwa ajili ya michezo kwenye kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) huku Mukoko Tonombe akiitwa kwa mara ya pili kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Congo DR. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Yacouba ambaye yupo Yanga kwa msimu wake wa kwanza ambapo mpaka sasa ameshatupia bao saba kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kwa upande wa Mukoko ambaye alijiunga na Yanga akitokea AS Vita Club ya Congo DR ameitwa kwa mara ya pili kufuatia kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu Bara akiwa na klabu yake ya Yanga.

Mukoko Tonombe mchezaji wa Yanga na Timu ya Taifa ya Jamhuri ya Congo

Wachrzaji hao watajiunga hivi karibuni kwenye timu zao mara baada ya kumalizika kwa mchezo war obo fainali ya michuano ya kombe la shirikisho (FA) dhidi ya Mwadui FC utakaochezwa kwenye Uwanja wa Ccm Kambarage Shinyanga.

error: Content is protected !!