July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ya Tundu Lissu yatimia

Jaji Augustino Ramadhani (kushoto) alipowasili mjini Dodoma kuchukua fomu ya kuwania urais

Spread the love

ILE kauli kuwa, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinavuruga katiba ya nchi kwa kuteua makada wake kutumikia serikali kinyume na Katiba ya nchi imetimia. Anaandika Benedict Kibache … (endelea). 

Katika Bunge la 10, Mkutano wa 19 kikao cha nane kilichofanyika Machi mwaka huu, Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu alililalamikia bunge kuwa, serikali imekuwa ikishindwa kutenganisha utumishi wa umma na utumishi wa chama kwa kuteua makada wake kutumikia serikali na CCM kwa wakati mmoja. 

Tayari baadhi ya watumishi wa umma walikuwa wakibanwa na Katiba kutokuwa wanachama wa chama chochote cha siasa, wamejitokeza na kudai ni wanachama halali wa chama cha siasa akiwemo aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustino Ramadhani. 

Yafuatayo ni maneno ya Lissu aliyoyatamka katika Bunge la 10, Mkutano wa 19 kikao cha nane kilichofanyika Machi mwaka huu;-   

Mheshimiwa Mwenyekiti; Serikali hii ya CCM inaweza ikawa inaandaa mazingira ya kisheria ya kuwa na au kuingiza au kuhalalisha uwepo wa makada wa CCM katika taasisi ya Dola, zinazokataza uanachama wa vyama vya siasa, sio hofu au dhana njama (conspiracy theory) isiyokuwa na msingi wowote.

Itakumbukwa kwamba, mwaka 2012 Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge (KRUB) lako tukufu ilihoji uhalali wa wanajeshi kuteuliwa kuwa Wakuu wa Wilaya. 

Kambi rasmi ya upinzani ilisema yafuatayo, naomba kunukuu:-

“Wakuu wa Wilaya na Mkoa wote ni wanachama wa CCM, hii ni kwasababu tangu kuanzishwa kwake mwaka 1977 wakuu wa wilaya wamekuwa wajumbe wa vikao vyote vikuu vya CCM katika ngazi ya wilaya. 

Kwa mfano kwa mujibu wa Katiba ya CCM toleo la 1982, Mkuu wa Wilaya ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya, ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya na ni Mjumbe wa Halmashauri ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Wilaya.

Hata baada ya miaka 30 tangia toleo hilo la kikatiba, kutolewa na licha ya miaka 20 ya vyama vingi vya siasa nchini hali ipo vilevile kuhusiana na nafasi ya wakuu wa wilaya kwenye vikao vya CCM.

Ndio maana kwa mujibu wa toleo la Katiba ya CCM la mwaka 2010, Mkuu wa Wilaya ni mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya, ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya na ni Mjumbe wa Halmashauri ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Wilaya. 

Naomba nirudie mheshimiwa mwenyekiti, kuwa Wakuu wa Wilaya ni mawakala wa utumishi wa umma kwa mujibu wa mkataba tunaoombwa kuuridhia leo.

Mheshimiwa mwenyekiti, licha ya utata wa kikatiba unaoruhusu wanajeshi kuwa wakuu wa wilaya na mikoa na hivyo kulazimika kuwa wanachama wa CCM na washiriki wa vikao vyake mbalimbali vya maamuzi serikali hii ya CCM imeendelea kuwachagua wanajeshi kwenye nafasi hizo kama uteuzi wa hivi karibuni wa Zelote Stephen ambaye miaka michache iliyopita alikuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa, kuwa Mkuu wa Wilaya. 

Aidha sasa kuna hofu ya msingi kwamba, hata majaji wetu wakuu wanaweza wasiwe salama sana. Kama taarifa za hivi karibuni za vyombo vya habari vilivyomuhusisha aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Agustino Ramadhani na mbio za kuwania urais kwa tiketi ya CCM kwenye Uchaguzi Mkuu baadae mwaka huu zitakuwa za kweli.

Kwa niaba ya kambi ya upinzani ya Bunge la lako tukufu kwa masharti ya ibara ya 3 sura ya 4 ya mkataba huu. Itakuwa ni halali sasa kwa mawakala hawa wa utumishi wa umma kuwa wanachama wa CCM, licha ya marufuku zilizoko kwenye ibara za 74, 14, 113a na 147 (3) za katiba. 

Kwa sababu hiyo kambi rasmi ya upinzani ya Bunge lako tukufu , inamuomba mtoa hoja kutoa ufafanuzi juu ya mgongano huu wa wazi kati ya matakwa ya mkataba tunaoombwa kuuridhia na masharti tajwa ya Katiba yetu.

error: Content is protected !!