August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Woodburn avunja rekodi ya Owen

Ben Woodburn, kinda la Liverpool aliyevunja rekodi ya Michael Owen

Spread the love

KINDA wa klabu ya Liverpool, Ben Woodburn (17), ameweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga goli akiwa na umri mdogo katika historia ya klabu hiyo toka kuanzishwa kwake, anaandika Kelvin Mwaipungu.

Woodburn ameweka rekodi hiyo akiwa na umri wa miaka 17 na siku 45 baada ya kufunga goli katika mchezo ambao Liverpool waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Leeds United kwenye hatua ya robo fainali ya Kombe la Ligi.

Awali rekodi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo Michael Owen aliyeiweka mwaka 1997 dhidi ya Wimbledon akiwa na umri wa miaka 17 na siku 98 na rekodi hiyo ilidumu kwa miaka 13.

Baada ya Woodburn kuweka rekodi hiyo jana usiku, Owen alimpongeza mchezaji huyo kupitia ukurasa wake wa kwenye mtandao wa Twitter saa chache baada ya mchezo kumalizika kwa kuweka rekodi hiyo.

error: Content is protected !!