January 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

WMA kuendesha ukaguzi

Kaimu Meneja wa Elimu, Habari na Mawasiliano wa Wakala wa Vipimo (WMA), Irene John akitoa elimu kwa mwananchi ya upimaji wa mita za maji

Spread the love

WAKALA wa Vipimo nchini (WMA), utaendesha ukaguzi na upimaji wa mita za maji Julai mwaka huu, kujua kama zinafanya kazi kwa usahihi. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Upimaji huo katika mita za maji utafanyika kwa mara ya kwanza nchi nzima, lengo likiwa ni kumlinda mlaji na serikali kutoza kodi sahihi kulingana na kiasi sahihi cha huduma inayotolewa.

Kauli hiyo imetolewa na Irene John, Kaimu Meneja Sehemu ya Elimu Habari na Mawasiliano wa WMA, wakati kizungumza na MwanaHALISI Online Ieo katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam.

“Julai mwaka huu, tunaanza kuhakiki mita za maji nchi nzima. Maeneo yanayohusika ni ya kibiashara na mita zinazotolewa na DAWASCO. Zoezi hili litakuwa endelevu,”ameeleza Irene.

Amesema kama mita hizo zitabainika kutofanya kazi kwa usahihi, watamshauri mtumiaji kutumia mita sahihi. Na kama itabainika mtumiaji wa mita anahujumu mapato ya serikali hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Aidha, amesema hatua hiyo, inakuja baada ya WMA kuimalika kwa kupata vifaa vya ukaguzi vya kisasa, kuongezeka kwa elimu, uwepo wa kanuni ya maji ambayo itatumika na kuongezeka kwa rasilimali watu.

“Tumejipanga kuhakikisha zoezi linafanikiwa. Tuna ofisi kila mkoa hapa nchini. Rai yatu wananchi watoe taarifa ili wakala tuweze kuzifanyia kazi,”amesema Irene.

error: Content is protected !!