Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari WLC kumuokoa mfanyabiashara na korona
Habari

WLC kumuokoa mfanyabiashara na korona

Spread the love

 

KAMPUNI ya Usafirishaji ya World Logistics (WLC), imeanzisha huduma mpya ya kuagiza na kufikishia bidhaa kwa mteja (Corgo Pickup & Delivery Services), ili kukabiliana na changamoto za korona (Uviko-19) kwa wafanyabisahara, wajasiriamali na kampuni kufuata bidhaa nje ya nchi. Anaripoti Selemani Msuya…(endelea).

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa WLC, Agnes Daniel wakati akizungumza na waandishi wa habari jana Ijumaa tarehe 3 Septemba 2021, jijini Dar es Salaam.

Ofisa Masoko huyo alisema wamekuja na huduma hiyo hasa katika kipindi hiki cha Janga la Uviko-19 ambalo limekuwa na athari kwa waagizaji na wafanyabiashara nchini.

Daniel alisema tangu kutokea janga la Uviko-19, biashara ya uagizaji mizigo au bidhaa mbalimbali ikishuka hivyo wanaamini njia hiyo mpya itaweza kusaidia waagizaji na wafanyabiashara kutoka kwenye janga la kuyumba kibiashara.

“Wakati dunia bado inahangaka na janga la Uviko-19, tumeamua kushiriki kwa kurahisisha kwa kulinda afya za Watanzania ambao wanaagiza au kufuata bidhaa nje kwa kuwaletea huduma hii ya Cargo Pickup & Delivery Service,” alisema.

Alisema kupitia huduma hiyo WLC watafuata mzigo au bidhaa ya mteja kiwandani, watafunga na kusafirisha hadi kwa muagizaji bila yeye kusumbuka.

Ofisa Masko Mkuu huyo alisema kupitia huduma hiyo muagizaji ataondokana na gharama za kusafiri, hoteli na michakato mingine ambayo inagharimu muda na fedha huku akibaki salama dhidi ya maambukizi ya Uviko-19.

Daniel alitoa wito kwa wafanyabiashara, wajasiriamali na Watanzania kwa ujumla ambao wanahitaji kuagiza bidhaa kutoka nje watumie WLC ambayo ni kampuni ya kizalendo.

Naye Ofisa Masoko, Apaisaria Godvice alisema kupitia huduma hiyo wanaamini mzunguko wa biashara utakuwa kwa kasi hivyo kusaidia lengo la Rais Samia Suluhu Hassan kuipeleka Tanzania katika uchumi wa kati kufanikiwa.

Godvice alisema wameeamua kuenda na teknolojia ili kuhakikisha ajira ambazo zipo zinakuwa endelevu hivyo ni imani yao wateja wao wataitumia huduma hiyo katika kufanya kuagiza bidhaa nje ya nchi.

“Sisi tunaagiza mizigo kutoka China, Uingereza, Japan, Afrika Kusini, Falme za Kiarabu, India, Malaysia na kwingineko. Lakini pia tunasafirisha mizigo kwenda duniani kote,” alisema.

Alisema katika kipindi cha miaka 15 ya WLC kutoa huduma wameweza kufikia wajasiriamali, wafanyabishara, makampuni na watu binafsi wengi hivyo lengo ni kuendelea kusaidia makundi hayo ili kukuza uchumi wa Tanzania.

Ofisa huyo alisisitiza kuwa pamoja na kuagiza mizigo na bidhaa kwa njia ya meli pia wanatumia usafiri wa ndege na barabara kuagizza na kusafirisha mizigo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariHabari Mchanganyiko

CRB yashtukia makandarasi wanaofanya ubia wa ujanja ujanja, yasema watakaobainika kuchukuliwa hatua kali

Spread the love  BODI ya Usajili wa Makandarasi (CRB), imeonya makandarasi wanaofanya...

HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love  MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba...

Habari

Mnyika aacha ujumbe msibani kwa kada wa Chadema aliyefia vitani Ukraine

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Taifa, John...

HabariHabari Mchanganyiko

Mwili wa kada wa Chadema aliyefia vitani Ukraine wawasili, kuzikwa Mbeya

Spread the loveMWILI wa Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, aliyefia...

error: Content is protected !!