May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wizkid aachia Deluxe Edition ya albamu ya Made in Lagos

Spread the love

 

MSANII wa muziki kutoka Nigeria, Ayodeji Ibrahim Balogum ‘Wizkid’, leo ameachia Deluxe Edition ya albamu yake ya ‘’Made in Lagos.’’ Anaripoti Glory Massamu, TUDARCo … (endelea).

Wizkid  katika albamu hiyo ameongeza ngoma mpya nne ambazo ni Anoti, Mood, Steady pamoja na Essence remix, aliyofanya na msanii Tems na Justine Bieber kutokea nchini Marekani.

Kabla ya Deluxe Edition, albamu hiyo ilikuwa na nyimbo 14, lakini iliyotoka sasa ina jumla ya nyimbo  18 baada ya kuongezeka nne.

Wizkid

Wizkid amedhibitisha kuachia albamu hiyo mpya kupitia ukurasa wake wa Instagram leo  kuwa albamu hiyo imeingia sokoni rasmi leo.

Hata hivyo siku kadhaa zilizopita nyimbo ya Essence ilipata nafasi ya kupanda kwenye chati za Billboard. Lakini pia inafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya radio na televisheni duniani kote. Kusababisha mashabiki wa msanii  huyo kufikiri kwamba kuna uwezekano wa Wizkid kufanya vizuri kwenye tuzo za Billboard msimu ujao.

error: Content is protected !!