Saturday , 3 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Wizi wamuibua JPM  
Habari Mchanganyiko

Wizi wamuibua JPM  

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS John Maguifuli amesema kuwa amebaini zaidi ya shilingi bilioni 1 walizodhulumiwa wananchi za mauzo ya korosho na vyama vya ushirika mkoani Mtwara. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Ameyasema hayo leo tarehe 20 Oktoba wakati anamuapisha ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama Naibu Katibu Mkuu wa Tamisemi na Balozi.

Rais Magufuli amewaapisha Mathias Kabunduguru kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya piaGodfrey Mweli kuwa Naibu Katibu Mkuu Tamisemi (anayeshughulikia elimu).

Rais Magufuli amesema kuwa awali alijua kuwa ni vyama vya ushirika  10 pekee ndivyo vilivyowadhurumu wananchi lakini alipomuagiza Brigedia Jenerali John Mbungo kufanya uchunguzi alibaini kuwa ni zaidi ya vyama 32 vimefanya uovu huo na kwamba alidhani kiasi cha shilingi 80 milioni pekee ndizo walizodhulumiwa wananchi kumbe ni zaidi ya bilioni moja.

“Kazi  hizi lazima tuwatumikie wananchi wanyonge juzi nilikuwa mtwara  tulikuta malalamiko … baadhi ya watu ambao wamedhurumiwa malipo yao ya korosho tangu mwaka 2016 hadi 2017 hawajalipwa na vilikuwa vyama vya ushirika kumi baada ya kumuagiza Brigedia Jenerali  Mbungo vyama vya ushirika 32 ambavyo vilivyokuwa vikiwadhurumu watu” amesema.

Amesema kuwa viongozi wa vyama vya ushirika wametiwa mikononi na kwamba wameanza kurejesh pesa za wanachi  “… ameweza kushika viongozi wa AMCOSi  92 na mpaka juzi walipokuwa wakinipa taarifa zilikuwa zimepatika Milioni 255 na zile nyingine zitarudishwa”

“Kwa hiyo munaweza kuona mtu amelima korosho yake ameuza amedhurumiwa na vyama vya ushirika tangu mwaka 2016/2017 anadai ameshakata tama zaidi ya bilioni moja zilikuwa ndani kwa viongozi wa AMCOS  na vyama vya ushirika unaweza kuona namna gani dhuruma inatendeka kwa wananchi hasaa wanyonge…tunajukumu la kutetea hawa wanyonge na kutoa machozi yao”

Magufuli amesema kuwa “Hii ni mifano tu saa nyengine katika kazi  hizi uongozi zinahitaji uvumilivu zinahitaji  mungu kumtanguliza mbele utasemwa saa nyengine usisemwe vizuri lakini hiyo ndio kazi uongozi kazi ya uongozi ni pamoja na kuchafuliwa” Amesema Rais Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Magunia 731 ya bangi yakamatwa, mamia ya hekari yateketezwa Arumeru

Spread the love  MAMIA ya magunia ya madawa ya kulevya aina ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Habari Mchanganyiko

Serikali yakabidhi eneo la mahakama ya Afrika ya haki za binadamu

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa...

Habari Mchanganyiko

Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2 bilioni

Spread the loveBENKI ya NMB imeendelea kufanya kazi kwa karibu na Asasi...

error: Content is protected !!