August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Wizi wa mtandao ni tatizo’

Spread the love
BENKI ya Posta Tanzania imeeleza kuwepo kwa changamoto kubwa katika kukabiliana na wizi wa fedha kwa njia ya mtandao hapa nchini, anaandika Dany Tibason.

Hayo yamebainishwa leo mjini Dodoma na Sabasaba Moshingi, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo alipokuwa akijibu hoja ya Japhet Hasunga, Mbunge  wa Vwawa (CCM) katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

Hasunga alitaka kujua benki hiyo imejipangaje katika kukabiliana na wizi wa fedha kwa njia ya mtandao ili fedha za wateja zibaki kuwa salama?

Akijibu hoja hiyo Sabasaba amesema, wizi huo ni changamoto kubwa kwa benki nyingi na wizi huo ufanyika kupitia  mashine za kutolea fedh (ATM).

Hata hivyo amesema, katika mpango mzima wa kukabiliana na wizi huo benki inajiandaa kuweka mfumo ambao utaweza kudhibiti wizi huo.

Mbali na hilo wabunge walitaka uongozi ueleze ni kwa jinsi gani wamekuwa wakiwasaidia wateja wao katika kuwakopesha hasa wale wa kipati cha chini.

Ayeshi Hilary, mwenyekiti wa kamati hiyo amesema, ili benki hiyo iweze kuwa na tija kwa jamii kama Shirika la Umma, ni lazima iweze kukopesha vikundi vya wafanyabiashara ndogo ndogo hususani vikundi vya akima mama na vijana.

Akizungumzia kuwapatika mikopo wafanyabiashara ndogo ndogo Leticia Ishengoma, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta Leticia amesema, benki hiyo imekuwa na utaratibu wa kukopesha makundi hayo tena kwa riba nafuu.

Laulence Mafuru, Msajili wa Hazina amesema, yapo mashirika mengi ya umma yakishindwa kujiendesha na kwamba, si sahihi.

Mafuru amesema, umefika wakati wakati wa mashirika ya Umma kujiendesha kwa faida na kama yapo katika mfumo wa biashara wafanye hivyo.

error: Content is protected !!