September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wizi wa kura 2015: Msigwa ‘amkomalia’ Spika Tulia

Spread the love

MCHUNGAJI Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini ameanzisha upya mjadala wa wizi wa kura, wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mbele ya Dk. Tulia Ackson, Naibu Spika, jana tarehe 6 Novemba 2019, Msigwa alisema kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, kulikuwa na wizi mkubwa wa kura, kauli ambayo iliikera serikali.

Kauli ya Msigwa ilimwinua Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ambapo aliomba mwongozo wa kiti cha spika, akilalamikia kauli ya Msigwa kwamba inaashiria kuwa wabunge wote hawana uhalali wa kuwa wabunge.

Mhagama alisema, kauli ya Msigwa imevunja kanuni na taratibu za Bunge, Katiba na Sheria.

Dk. Tulia alimtaka Msigwa kufuta kauli yake kabla ya hatua zingine kuchukuliwa, hata hivyo Msigwa aligoma kufuta kauli hiyo na kubaki kwenye msimamo wake ule ule.

Hatua hiyo ilimsukuma Dk. Tulia kumtaka Msigwa kufika mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhojiwa ili kuthibitisha madai yake.

error: Content is protected !!