September 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wizara yazitaka mamlaka kutafuta masoko kimataifa

Spread the love

WIZARA ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki nchini Tanzania, imeshauri mamlaka kutembelea nchi za kimkakati kwa kuzingatia maslahi ya nchi hiyo katika nchi mbalimbali. Anaripoti Glory Massamu, TUDARCo…(endelea)


Hayo yamesemwa na naibu waziri wa wizara hiyo, Balozi Mbarouk Nasser Mbarouk wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbarali (CCM), Francis Mtega aliyeuliza ni lini viongozi wa kitaifa wataanza kutembelea nchi za nje mahususi kwenda kutafuta masoko ya mazao hususani mpunga na mahindi.

Balozi Mbarouk amesema, vingozi wameanza kutembelea nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na zile za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

“Mei 2021, wizara iliratibu ziara ya kikazi ya Rais Samia Suluhu kwenda Kenya, Burundi, Rwanda na Uganda,” amesema

Aidha amesema ziara za viongozi wa Kitaifa nje zimekuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na nchi rafiki.

“Rais Samia alipokwenda nchini Kenya alifanikiwa kutanzua vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiforodha (NTBs) vilivyokuwa vinawakabili wafanyabiara wa mahindi kwenda Kenya.”

Hata hivyo, Rais Samia alitumia fursa ya ziara hizo, kutafuta masoko ya bidhaa za mazao kutoka Tanzania ikiwemo mahindi, mpunga na marahage ameyasema hayo.

Balozi Mbarouk amesema, “hivi sasa tayari wizara ya mambo ya nje imeunda idara maalumu ya ‘economic diplomacy’ ambayo itashughulikia swala la masoko.”

error: Content is protected !!