January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wizara yalalamikia kampeni ya WHO

Tumbaku ikiwa imeanikwa

Spread the love

WIZARA ya Kilimo, Chakula na Ushirika imelalamikia kampeni zinazofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuwa, zimesababisha kushuka kwa bei ya tumbaku nchini. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi amesema, bei ya tumbaku katika soko la dunia imekuwa ikibadilika mara kwa mara kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ushindani wa uzalishaji na ubora wa tumbaku kwa nchi zinazozalisha tumbaku duniani.

Amesema udhibiti wa bidhaa za tumbaku na matumizi yake unaofanywa na WHO kupitia Kampeni ya Framework Convention on Tobacco Control (FCTC), umesababisha pia kushuka kwa matumizi ya bidhaa hizo na hivyo kuathiri bei ya zao hilo kwa wakulima nchini.

Amesema kutokana na hali hiyo, serikali itaendelea kutafuta masoko ya tumbaku katika nchi mbalimbali ili kuwezesha wakulima kuuza zao hilo kwa bei nzuti na hivyo kupata faida.

Katika kukabiliana na changamoto ya kupanda na kushuka kwa bei za mazao ya biashara katika soko la dunia ikiwemo zao la Tumbaku, wizara kwa kushirikiana na wadau wa mazao husika inaandaa utaratibu maalum wa kufidia bei za mazao kwa ajili ya kuwasaidia wakulima pindi mazao yanaposhuka katika Soko la Dunia.

Naibu waziri huyo alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Mpanda Vijijini (CCM), Moshi Kakoso ambaye alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuwafidia hasara waliyoipata wakulima wa zao la tumbaku nchini baada ya zao hilo kushuka bei katika soko la Dunia.

error: Content is protected !!