January 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wizara ya Mawasiliano yasikia kilio cha wananchi

Spread the love

WIZARA ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia imewataka wananchi kujenga tabia ya kutoa malalamiko kwa wakala wa mitandao ya simu na Mamlaka ya Mawasiliano ili kutatua vikwazo vya kuunganishwa katika huduma za simu bila ridhaa zao. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Hayo yamesemwa leo na Msemaji wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknologia, Prisca Ulomi katika mazungumzo yeke na wanahabari Jijini Dar es Salaam kuhusu kanuni mpya za huduma za ziada za 2015.

Ulomi amesema kanuni hiyo iliyoanza kutumika Agosti 7 mwaka huu, inampa fursa mtumiaji wa huduma za ziada wa mitandao mbalimbali kujiridhisha na huduma zinazoanzishwa na kufanya changuo ili kuondokana na adha ya kuunganishwa katika huduma bila taarifa.

Amesema kuwa, kanuni hiyo inamtaka mtoa huduma kutoa taarifa kamili na sahihi kwa lugha rahisi ambazo ni Kiswahili na Kingereza pamoja na kutia masharti na vigezo vya huduma husika.

“Suala la malalamiko ya kuunganishwa katika huduma bila ridhaa limesikika sana hivyo kutokana na malalamiko hayo kuwa ni janga la taifa, wizara imeweka kanuni mpya zitakazosimamia watoa huduna na watumiaji,” amesema Ulomi.

error: Content is protected !!