January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Wizara ya Maji inanuka ufisadi’

Mabomba ya maji

Spread the love

KAMBI ya upinzani imesema kuwa, Wizara ya Maji imeghubikwa na ufisadi wa kutisha hususan kupitia miradi ya vijiji 10 kwa kila wilaya. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Hayo yalielezwa jana bungeni na Msemaji wa Kambi Rasim ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Maji, Rajab Mbarouk Mohammed wakati akiwasilisha hotuba ya Wizara ya Maji kuhusu mapitio ya utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2014/2015 na makadirio ya mapato na matumizi ya wizara kwa mwaka wa fedha 2015/16.

Mbarouk amesema kuwa, ufisadi huo umejithihirisha katika miradi ya maji kwenye vijiji 10 kwa kila wilaya inayofadhiliwa na Benki ya Duni tangu 2007 imeendelea kuwa kitendawili hapa nchini. 

Amesema, bajeti ya mwaka jana 2014/2015 serikali ilitenga fedha na Bunge likapitisha kwa ajili ya kukamilisha miradi hiyo ambayo ni kero kubwa kwa wananchi. 

Pamoja na bunge kupitisha fedha hizo amesema, hakuna kilichofanyika kusogeze mbele miradi ambayo kwa kiasi kikubwa mingi kukwama. 

Amesema kuwa, zaidi ya asilimia 75 ya miradi ya Benki ya Dunia ambayo ilionekana kuleta matumaini makubwa kwa wananchi, imeshindwa kutekelezeka na kukwama na kwa tukio hilo ni aibu kwa taifa. 

Mbarouk amesema, lengo la miradi hiyo kwa wananchi lilikuwa ni zuri lakini kutokana na udhahifu wa kiutendaji miradi hiyo imekuwa ni kichaka cha kujificha kwa wabadhirifu wa fedha za maji. 

“Kitendo cha kutekeleza miradi ya aina moja kwa halmashauri zile zile na watendaji wale wale ni tatizo kubwa, lakini kwa kuwa wahusika wakubwa ngazi za juu nao ni sehemu ya ufisadi huo inakuwa vigumu sana kubadilisha mfumo na kuthibiti wizi huo,” amesema.

Mbali na kukosekana kwa maji Mbarouk alisema kuwa serikali imekuwa na tabia ya kuzindua miradi ya maji ambayo inafanya kazi kwa muda mfupi na kufa au wakati mwingine haina maji kabisa.

Amesema, ufisadi huo ndio unasababisha kuwepo kwa miradi mingi ya maji hewa huku serikali ikiendelea kunyamaza kimya.

error: Content is protected !!