Wednesday , 6 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Wizara ya madini kurusha ndege ya utafiti wa madini Geita
Habari Mchanganyiko

Wizara ya madini kurusha ndege ya utafiti wa madini Geita

Spread the love

Kutokana na mchango wa wachimbaji wadogo wa madini kwenye pato la Taifa, Wizara ya madini inatarajiwa kufanya utafiti wa kina kwa kurusha ndege maeneo mbalimbali ikiwemo mkoani Geita ili kupata taarifa sahihi za uwepo wa madini katika maeneo husika. Anaripoti Mwandishi Wetu …(Geita).

Hayo yamebainishwa jana tarehe 25 Septemba 2023 na  Waziri wa Madini, Anthony Mavunde wakati akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini mkoani Geita katika kongamano la kuibua fursa za madini pamoja na kujadiliana juu ya changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo.

Mavunde aliongeza kuwa Wizara ya Madini ipo katika mkakati wa kuongeza taarifa za utafiti wa kina wa madini kwa lengo la kufungamanisha sekta ya madini na sekta nyingine za kiuchumi.

Akifafanua kuhusu hali ya utafiti nchini, Mavunde alisema kuwa kwasasa Serikali imefanya utafiti wa kina kwa asilimia 16 ya eneo la nchi  ambayo taarifa zake  ndizo zinazotumika  kuendeleza  miradi ya uchimbaji madini.

Vilevile, Mavunde aliongeza kuwa kutokana na umuhimu wa taarifa hizo Serikali imepanga ifikapo mwaka 2030 iwe imefanya utafiti wa kina nchi nzima ili kubaini  maeneo yote yenye rasilimali madini, hii itasaidia kuongeza wigo kwa wachimbaji wadogo, wakati na wakubwa tofauti na ilivyo sasa.


Akielezea kuhusu mchango wa sekta ya madini katika pato la Taifa, Mavunde alisema sekta ya madini inaendelea kupaa na  mpaka sasa inachangia kiasi cha  asilimia 9.1, hii ni kwa taarifa za utafiti wa asilimia 16 tu, hivyo kwa kuongeza taarifa za kina sekta ya madini itakuwa kinara katika uchangiaji katika sekta hiyo.

Awali katika kongamano hilo Taasisi zilizochini ya wizara ya madini ziliwasilisha mada mbalimbali juu ya mnyororo mzima wa sekta ya madini ikiwa pamoja na mpango wa kuwainua wachimbaji wadogo ili wafanye uchimbaji wenye tija na uhakika.

Kongamano hilo lilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa Geita, Mbunge wa Geita Mjini,Taasisi za Fedha, Wakuu wa Taasisi za Umma na viongozi wa Vyama vya  Wachimbaji wadogo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Shura ya Maimamu kukata rufaa kupinga Sheikh kufungwa miaka 7

Spread the loveSHURA ya Maimamu Tanzania, inakusudia kukata rufaa dhidi ya hukumu...

Habari Mchanganyiko

TMA yaagizwa kutangaza mafanikio yao kikanda, kimataifa

Spread the love  KATIBU Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara ameiagiza...

Habari Mchanganyiko

NMB yasaidia waathirika wa mafuriko, maporomoko Hanang

Spread the loveWaathirika wa maporomoko ya tope Wilayani Hanang, mkoani Manyara, waliopoteza...

Habari Mchanganyiko

TPF-NET Arusha yaonya jamii ya wafugaji zinazoendeleza ukatili wa watoto na wanawake

Spread the love  MTANDAO wa Polisi wanawake wa Arusha kuelekea siku 12...

error: Content is protected !!