Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Biashara Wizara ya Kilimo, NMB zatangaza neema sekta ya kilimo
Biashara

Wizara ya Kilimo, NMB zatangaza neema sekta ya kilimo

Afisa Mkuu wa Wateja binafsi na Biashara Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kushoto) akimpa maelezo Waziri wa Kilimo, Husein Bashe (katikati) jinsi NMB ilivyojipanga kuhudumia kilimo mara baada ya kutangaza Makubaliano ya kushusha riba ya mikopo kwa wakulima,wavuvi na wafugaji kwa asilimia tisa, kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna. Makubaliano hayo yalifanyika jijini Dodoma jana
Spread the love

WIZARA ya Kilimo na Benki ya NMB za nchini Tanzania, wameingia makubaliano ya kukuza sekta ya kilimo nchini humo ambapo benki hiyo imetenga Sh.20 bilioni kwa ajili ya kutoa mikopo ya ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mazao hasa maeneo ya vijijini na Sh.100 bilioni kwa ajili ya kukuza kilimo nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Akizungumza katika hafla ya makuliano hayo iliyofanyika jana Jumanne tarehe 12 Aprili 2022, jijini Dodoma, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna alisema wamekubali kuingia makubaliano hayo baada ya mazungumzo ya muda mrefu kati ya benki hiyo na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe.

Alisema mikopo hiyo ya ujenzi wa maghala, itatolewa kwa riba nafuu ya asilimia 9 na mazao yanayolengwa kwa kuanzia ni korosho, pamba na nafaka.

Alisema mkopo huo ni mwendelezo wa juhudi ya NMB kukuza sekta ya kilimo nchini kwani Oktoba 2021, benki hiyo ilitenga Sh.100 bilioni kwa ajili ya kukopesha sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi kwa riba isiyozidi asilimia 10.

“Kwa taarifa tu, mpaka sasa zaidi ya Shilingi Bilioni 80 zimeshatolewa kwenye mikopo hii. Baada ya kuona shilingi bilioni 100 zinaisha, leo tunaona tuongeze nyingine kama hizo ili kuongeza utoaji wa mikopo kwa wakulima, wavuvi, wafugaji na wajasiliamali katika sekta hizi huku tukipunguza riba ya mikopo hii mpaka asilimia 9,” alisema Zaipuna.

Waziri wa Kilimo na Chakula, Hussein Bashe (katikati) akimpongeza Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (kulia) kwa juhudi zake za kusaidia ukuaji wa sekta ya kilimo nchini mara baada ya kutangaza kushusha riba ya mikopo kwa wakulima,wavuvi na wafugaji ambayo sasa itakuwa asilimia 9. Kushoto ni fisa Mkuu wa Wateja binafsi na Biashara Benki ya NMB, Filbert Mponzi. Makubaliano hayo yalifanyika jijini Dodoma wiki hii

Alisema nyongeza hiyo ya shilingi bilioni 100 kwenye mikopo na shilingi Bilioni 20 kwenye ujenzi wa maghala, kunafanya kiasi ambacho tayari kimetengwa na NMB kwa ajili ya mikopo nafuu ya kilimo kufikia Shilingi Bilioni 220.

“Leo tupo hapa na waziri wa kilimo Mh Hussein Bashe ili kuwatangazia makubaliano tuliyofikia kati ya wizara ya kilimo na benki ya NMB yanayolenga kuendeleza juhudi za kukuza kilimo nchini,” alisema

“Tumekuwa na mazungumzo kadha na Mh Waziri toka alipoteuliwa kuwa waziri wa kilimo. Kwetu kama Benki ilikuwa ni muhimu sana kuonana na kuelewa maono ama vision aliyonayo waziri kwenye sekta ya kilimo kama waziri mwenye dhamana ili sisi tuweze kuona ni jinsi gani tutaingia kusaidia kutekeleza maono hayo,” alisema Zaipuna

Alisema moja ya changamoto kubwa waliyoongea na Waziri Bashe inayowakabili wakulima vijiini ambayo NMB wanaweza kusaidia kutatua kwa sehemu ni ukosefu wa maghala ya kuhifadhia mazao hasa maeneo ya vijijini.

Waziri wa Kilimo na Chakula, Hussein Bashe (katikati) akimpongeza Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (kulia) kwa juhudi zake za kusaidia ukuaji wa sekta ya kilimo nchini mara baada ya kutangaza kushusha riba ya mikopo kwa wakulima,wavuvi na wafugaji ambayo sasa itakuwa asilimia 9. Kushoto ni fisa Mkuu wa Wateja binafsi na Biashara Benki ya NMB, Filbert Mponzi. Makubaliano hayo yalifanyika jijini Dodoma wiki hii

“Ni matarajio yangu kuwa wakulima, wafugaji, wavuvi, wafanyabiashara na wajasiliamali katika tasnia hii watumie fursa hii kuendelea kujipatia mikopo nafuu na kujiongezea kipato na kujenga nchi yetu,’ alisema

Kwa mujibu wa Zaipuna, NMB itazingatia masharti ya utoaji wa mikopo hii nafuu kwa kuzingatia taratibu za ukopeshaji ikiwemo kiwango cha juu cha mkopo cha Sh.1 Bilioni kwa mkopaji mmoja.

Alisema mkopaji huyu anaweza kuwa mtu binafsi, chama cha ushirika, kampuni au taasisi yeyote itakayokidhi masharti ya ukopeshaji.

“Ninatoa wito kwa wanaotaka kukopa mikopo hii nafuu zaidi sokoni, kutembelea mtandao wetu wa matawi 226 yaliyo enea nchi nzima ili kuweza kupata huduma za mikopo hii ya riba nafuu,” alisema.

Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo, Bashe aliipongeza NMB kwa juhudi zake za kukuza sekta ya kilimo nchini.

Alisema moja ya changamoto wanayokabiliana nayo wakulima vijijini ni mazao yao kupoteza ubora kabla ya kufika sokoni kutokana na mazingira mabaya ya kuhifadhi mazao yao.

“Kule vijijini ukiona magunia mengi ya mazao yamewekwa kwenye eneo la mashine za kusaga, usifikiri kuwa ni mali ya mwenye mashine hiyo. Magunia hayo ni mali ya wakulima yamehifadhiwa hapo baada ya kukosa ghala la kuhifadhia na yanapofika sokoni, yanakuwa yamepoteza ubora na thamani yake,” alisema Bashe.

Waziri Bashe alisema wizara yake inatambua matatizo na changamoto za wakulima na imejipanga kukabiliana nayo kwa kushirikiana na wadau kama Benki ya NMB.

Alisema maghala hayo yatajengwa kupitia vyama vya ushirika na Wizara ya kilimo itasimamia kuhakikisha dhamila ya Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kukuza sekta ya kilimo, inatimia.

Alisema maghala yatakayojengwa, yatakuwa na uwezo wa kuhifadhi tani 100, 200 hadi 300 ili wakulima waweze kutunza mazao yao na yabaki kwenye ubora kabla ya kufika sokoni.

2 Comments

  • NAHITAJI MKOPO KWA AJILI YA KUANZA UFUGAJI WA NG”OMBE WA MAZIWA WATANO NA KUJENGA MABANDA,ENEO LA HEKARI MOJA TAYARI NINALO

  • Ni jambo jema Sana. Serikali isimamie ipasavyo Ili kuisimamia harakati za ukuzaji wa uchumi wa Taifa. NMB pia mngetoa namba za mawasiliano Ili kurahisisha mawasiliano na wateja(WAKOPAJI) kwani Kuna watu wanaoishi mbali sana na matawini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Soko nepi za watoto lashuka, watu wazima lapaa

Spread the loveKiwanda cha kutengeneza nepi cha Japan kimetangaza kuwa kitaacha kutengeneza...

Biashara

Mchezo mpya mjini Super Heli Kasino, ushindi, zawadi ndiyo sehemu yake

Spread the love  KUNA watu wanakwambia hakuna njia rahisi ya mafanikio kwenye...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yafuturisha Unguja, Pemba, SMZ yaahidi ushirikiano

Spread the loveBENKI ya NMB imeendeleza utamaduni wa kufuturisha wateja wake walioko...

error: Content is protected !!