SERIKALI ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imejipanga kuchukua hatua stahiki katika kuhakikisha uchumi unaendelea kukukua kwa kusimamia urekebishwaji wa baadhi ya sera. Anaripoti Mwandishi WEtu, Dar es Salaam … (endelea).
Hayo yameelezwa katika mafunzo maalumu kwa wahariri wa vyombo mbalimbali kuhusiana na mwenendo wa uchumi wa Dunia na namna ambavyo Tanzania inavyoathiwa yaliyoandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) yaliyofanyika leo Januari 16, 2023 jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence Mafuru, amesema kuwa unapozungumzia uchumi wa Dunia ni lazima utaizungumzia maeneo makubwa matatu ambayo ni nchi ya China, Umoja wa Ulaya na Marekani kwa kuwa ni nchi ambazo uchumi wake ni mkubwa.
“Unapozungumzia uchumi wa Dunia huwezi kukwepa kuizungumzia China kwani ni nchini yenye uchumi mkubwa duniani lakini pia zipo nchi ambazo nazo ni lazima uzizungumzie unaelezea masuala ya uchumi duniani,” amesema Mafuru.
Amesema kuwa China inaposhuka uchumi wake kuna nchi ambazo huathirika na kusababisha changamoto mbalimbali kama kuibuka kwa mfumuko wa bei, kupanda kwa riba katika benki, changamoto ya ajira, kuwepo kwa vikwazo vya dunia.
Mafuru amesema mbali na China lakini mfumuko wa bei katika nchi za Umoja wa Ulaya na Marekani zimeathiri moja kwa moja uchumi wa dunia ambapo Tanzania ikiwa ndani yake.
Amesema kuwepo kwa vita kati nchi ya Ukraine na Urusi pia kumeathiri pia katika kushuka kwa uchumi wa dunia lakini pia suala la ugonjwa wa COVID nalo limethiri nchi nyingi duniani uchumi wake kushuka.
“Katika kipindi hiki cha COVID nchi nyingi uzalishaji wake ulishuka hivyo kumesababisha uchumi wa nchi nyingi kushuka kwani wananchi walikuwa lockdown, bidhaa kutosafirishwa na kutofanyika kwa biashara mbalimbali,” amesema.
Mafuru amesema kuwa ili kuhakikisha kuwa Tanzania uchumi wake unasonga mbele wamejipanga kutumia fulsa zilizopo ambazo ni usafirishaji wa bidhaa zinazopita nchini kuelekea mataifa jirani ambayo yamepakana na nchi hii.
Amesema hatua nyingine ambayo inaweza kutumina na kuinusuru Tanzania katika ukuaji wa uchumi ni kutumia utalii ambao kwa sasa umerudi katika hadhi yake baada ya kupungua kwa ugonjwa wa Uviko, lakini pia kukuza kilimo na uwepo na gesi asilia, madini mbalimbali.
Leave a comment