Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Wizara ya Elimu yaipa Zanzibar vishikwambi vya walimu 6,600
Elimu

Wizara ya Elimu yaipa Zanzibar vishikwambi vya walimu 6,600

Spread the love

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia leo Desemba 22, 2022 imetoa jumla ya vishikwambi 6,600 kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kwa ajili ya kugawa kwa walimu ili kuwapa motisha na kuvitumia kama vitendea kazi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Makabidhiano hayo yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam kati ya Dk. Francis Michael, Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Khamis Abdulla Said, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar na kuhudhuriwa na baadhi ya viongozi na maafisa wa Wizara hizo.

Katika hafla hiyo Dk. Michael amesema Kati ya vishkwambi 300,000 vilivyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya zoezi la Sensa ya watu na makazi iliamriwa vigawiwe katika sekta ya elimu ambapo vishkwambi 6,600 ni kwa ajili ya walimu Zanzibar.

“Huku Bara tuliwapa walimu vishkwambi kama motisha, yaani ni mali yao tukiamini watavitumia ipasavyo kama vitendea kazi muhimu na nyie mkifanya hivyo itakuwa ni vizuri kwa kuwa motisha kwa walimu ni kitu cha muhimu sana na ni agizo la Waziri Mkuu,” amesema Dk. Michael.

Ameongeza kuwa ni matarajio ya Serikali kuwa vishkwambi hivyo vitakuwa chachu katika kuboresha mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji ili kuinua ubora wa elimu nchini.

Naye Katibu Mkuu, Said ameshukuru kwa kupatiwa vishkwambi hivyo na kuahidi kuwapatia walengwa mara moja ili waanze kuvitumia kwa ajili ya kuwasaidia katika kazi ya ufundishaji wanafunzi.

“Nina furaha kubwa kupokea vishkwambi hivi na ninaamini vitaleta mapinduzi makubwa sana katika masuala ya Elimu kule Zanzibar. Nitahakikisha vinagawiwa kwa walimu kama ilivyoelekezwa ili matarajio ya Serikali yatimie,” amesema Said.

Kwa upande wake, Prof. Carolyne Nombo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia amesema katika maoni yanayopokelewa ya maboresho ya mitaala ni kuhusu uboreshaji somo la Tehama hivyo uwepo wa vishkwambi utakuwa ni msingi wa utekelezaji wa uimarishaji ufundishaji wa somo hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Waliopata Division one St Anne Marie Academy waula, Waahidiwa kupelekwa Ngorongoro, Mikumi

Spread the love WANAFUNZI wa shule ya St Anne Marie Academy waliofanya...

ElimuMakala & Uchambuzi

Waraka maalumu kwa NECTA, “hawapaswi kuungwa mkono”

Spread the loveHATUA iliyotangazwa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), ya...

Elimu

NACTVET yafungua dirisha la udahili

Spread the love  BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo...

Elimu

Prof. Mwakalila awafunda wanafunzi Chuo Mwalimu Nyerere, “ulipaji ada ni muhimu”

Spread the love  MKUU wa Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere (MNMA),...

error: Content is protected !!