Tuesday , 23 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wizara ya ardhi yanunua ‘drone’, yapima viwanja milioni 2.7
Habari Mchanganyiko

Wizara ya ardhi yanunua ‘drone’, yapima viwanja milioni 2.7

Spread the love

 

WIZARA ya Nyumba na Maendeleo ya Makazi imenunua ndege isiyokuwa na rubani (drone) maalum kwa ajili ya upigaji picha za anga zinazowezesha uandaaji wa ramani za msingi na kuzifanyia marejeo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kutokana na mfumo na vifaa vya kisasa, viwanja 2,783,278 na mashamba 28,784 yamepimwa nchini kote.

Hayo yameelezwa leo tarehe 21 Novemba, 2021 na Waziri mwenye dhamana William Lukuvi wakatin akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya wizara hiyo katika kipindi cha miaka 60 iliyopita tangu Tanzania bara ilipopata uhuru mwaka 1961.

Lukuvi amesema tangu wakati Tanganyika (Tanzania bara) inapata Uhuru kulikuwepo na sheria nyingi zilizorithiwa kutoka kwa wakoloni na sasa zimefanyiwa marekebisho.

Amesema sera na sheria hizo zilikua za kibaguzi nao zilishindwa kukidhi matarajio ya nchi baada ya uhuru.

“Hali hiyo ilipelekea kufanyika kwa mabadiliko ikiwemo kutunga na kufanya mapitio ya sera na sheria hizo ili kukidhi mahitaji ya wakati huo ikiwemo kuwezesha wananchi kumiliki ardhi, kuwezesha wananchi kiuchumi na kupunguza migogoro ya ardhi” amesema.

Aidha, Lukuvi amebainisha miongoni mwa sheria zilizotungwa au kurejewa ni sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995, Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Makazi ya mwaka 2000, Sheria ya Ardhi, Sura ya 113.

Lukuvi amesema baada ya kupata uhuru mwaka 1961, Serikali ilianza kuboresha mazingira ya uendelezaji milki nchini pamoja na kuanzisha Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mwaka 1962 kwa sheria ya Bunge Na. 45 kwa lengo lakuwapatia wananchi makazi bora.

Amesema Serikali ilianzisha wakala wa Ujenzi wa Nyumba na Majengo ya Serikali (TBA) na taasisi zingine za serikali zinajishughulisha na ujenzi wa ofisi na majengo mengine kwa shughuli mbalimbali za ofisi.

Aidha, ameeleza watu binafsi wanashiriki katika ujenzi wa nyumba za kuishi na biashara.

Amesema Shirika lina majengo 2,728 yenye sehemu ya nyumba (units) zipatazo 18,622 katika maeneo mbalimbali nchini na ina viwanja vipatavyo 2,561.

“Rasilimali hizi zinalifanya Shirika kuwa na utajiri wa mtaji (Capital base) wa shilingi trilioni 5.

“Nyumba za makazi ni asilimia 59 na za biashara ni asilimia 41. Katika jumla ya nyumba hizo, asilimia 59.3 ziko katika Jiji la Dar es Salaam.

“Nyumba hizi 18,708 zinaliingizia Shirika kodi ya wastani wa shilingi bilioni 8 kwa mwezi.

“Kwa sasa Shirika linaendelea kujenga nyumba za kuuza, kupangisha na biashara karibu kila mkoa na wilaya.

“Kwa upande wa Mkoa wa Dodoma Shirika linakamilisha ujenzi wa nyumba 1,000 Jijini Dodoma,” ameeleza Lukuvi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari Mchanganyiko

DC ampongeza Dk. Rose Rwakatare kwa kusaidia waathirika wa mafuriko Mlimba

Spread the loveMWENYEKITI wa Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk.  Rose Rwakatare...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!