Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Maisha Afya Wizara ya Afya yapokea mashine 100 za saratani
Afya

Wizara ya Afya yapokea mashine 100 za saratani

Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (kushoto) akiwa Naibu wake, Faustine Ndungulile
Spread the love

UMMY Mwalimu, Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, amepokea mashine 100 za tiba mgando (cryotherapy), mashine tisa za upasuaji mdogo (LEEP) kwa matibabu ya awali ya saratani kwa wanawake na mitungi 173 ya gesi carbon dioxide itakayowezesha mashine hizo kuweza kufanya kazi, anaandika Angel Willium.

Akiongea na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Ummy amesema tangu mwaka 2008 wizara yake ilianza kutoa huduma ya uchunguzi kwa kutumia siki (acetic acid) na matibabu ya mabadiliko ya awali ya saratani ya mlango wa kizazi kwa kutumia tiba mgando (cryotherapy).

“Wizara inawapongeza na kuwashukuru wadau wote wanaoshiriki katika kuimalisha upatikanaji wa huduma hizi, tungependa kuwatambua mchango wa Jhpiego, ICAP, EGPAF, THPS, MEWATA, T-Marc na WAMA,” amesema Ummy.

Ummy amesema anapenda kuwahimiza wanawake kujitokeza kwa wingi kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya awali ya saratani ya mlango wa kizazi katika vituo kwani huduma hizi zinatolewa katika kliniki ya afya ya mama na mtoto kila siku na bila malipo yoyote.

Aidha ameomba vituo vya umma kutenga siku maalumu katika kila mwezi ambayo kituo kitahamasisha wanawake kuja kwa wingi kupata huduma, na mwezi Oktoba kila mwaka uwe mwezi wa uhamasishaji wa upimaji wa saratani ya matiti Dunia kote.

Kwa upande wake, Dk. Robert J. Kamala kutoka katika kitengo cha Medical Consultant, ameeleza jinsi ya kutumia mashine ya tiba mgando (cryotherapy), amesema kabla ya kumpima saratani lazima mama aangaliwe kama ana tatizo lolote au mjamzito, ili kuondoa kwanza matatizo hayo ndiyo watibu saratani.

Takwimu za Taasisi ya saratani ya Ocean Road kwa kipindi cha mwaka 2006 hadi 2015 zinaonyesha kwamba aina ya saratani zinazoongoza ni saratani ya mlango wa kizazi 34% saratani ya kichwa na shingo 7%, saratani ya kibofu cha mkojo 3%, saratani ya matiti 12%.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

AfyaTangulizi

Wanasayansi wagundua teknolojia ya kunyofoa VVU kutoka kwenye seli

Spread the loveTIMU ya wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Amsterdam cha nchini...

Afya

Wananchi 530,000 kufaidika na ujenzi wa hospitali ya bil. 1.8

Spread the love  SERIKALI imetoa Sh 1.8 bilioni kwa ajili ya ujenzi...

error: Content is protected !!