June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wizara ya afya yajipanga kuchanja watu 600,000

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi

Spread the love

 

Wizara ya afya maendeleo, jinsia, wazee na watoto inatarajia kuzindua mpango wa kuharakisha chanjo ya Uviko-19 kuanzia tarehe 20 Septemba, 2021. Anaripoti Victoria Mwakisimba, TUDARCo … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu mkuu Wizara ya Afya Maendeleo, Jinsia, Wazee na Watoto, Abel Makubi amesema watu 600,000 watapata chanjo hadi kufikia tarehe 20 ya mwezi huu.

Amesema kuwa mpango huo utahusisha magari ya chanjo yanayo tembea na kufika kwenye maeneo mbalimbali nchini na idadi ya vituo vya chanjo itaongozeka hadi kufikia 6,784.

Aidha, Makubi amewaagiza maofisa wa matibabu wa wilaya na mikoa kote nchini kusimamia na kutekeleza zoezi hilo ili kuhakikisha watu wanapata chanjo.

Kampeni ya utoaji chanjo ya Uviko-19 ilizinduliwa rasmi nchini Tanzania na Rais Samia Suluhu Hassan na kuwahakikishia wananchi wake kuwa chanjo hizo ni salama.

error: Content is protected !!