Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Wizara ya afya: Tupande miti, tusafishe mazingira
Habari Mchanganyiko

Wizara ya afya: Tupande miti, tusafishe mazingira

Spread the love

 

NAIBU Waziri wa Afya nchini Tanzania, Dk. Godwin Mollel amewataka wataalam wa afya mazingira katika ngazi ya mkoa na halmashauri kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa wananchi juu ya umuhimu wa kupanda miti na kusafisha mazingira ili kuepusha jamii na magonjwa ya kuambukiza. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Dk. Mollel amesema hayo leo Alhamisi, tarehe 10 Februari 2022, wakati akizungumza na wananchi katika soko la Mavunde (Soko la Chang’ombe) baada ya kufanya usafi katika eneo hilo ikiwa ni sehemu ya zoezi endelevu la kuhamasisha wananchi kufanya usafi wa mazingira na kupanda miti.

“Sasa tunataka wataalam wetu wa halmashauri na mkoa muweke nguvu katika kutoa elimu na hamasa kwa wananchi kutunza mazingira pamoja na kupanda miti,” amesema.

Pia, Dk. Mollel amewataka wataalam hao kuhakikisha wanasimamia angalau kila mtu apande walau miti 20 kwa mwaka huku akisisitiza zoezi hilo liende mpaka kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

Naibu waziri huyo, amewahamasisha wananchi wa Dodoma kujenga utamaduni wa kupanda miti katika maeneo yao ya kuishi na maeneo wanayofanyia shughuli za kukuza uchumi ili kutunza mazingira na kupendezesha mji.

Dk. Mollel amesema moja kati ya visababishi vya kuongeza umri wa kuishi ni pamoja na kufanya usafi wa mazingira yetu ili kuzuia milipuko ya magonjwa kama vile Kipindupindu yanayoweza kupelekea kupoteza maisha kwa wananchi ambao hawafuati kanuni za usafi wa mazingira.

“Nawashukuru sana Watendaji mnaofanya kazi hii, mkifanya mazingira yenu kuwa mazuri gharama ya kusafisha mazingira ni kidogo kuliko gharama ya kwenda hospitali kwaajili ya kutibu magonjwa yanayotokana na mazingira yetu kuwa machafu” ameshukuru Dk. Mollel.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu-Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano, Mary Maganga amesema, katika kuelekea uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya Mwaka 2021, wizara yake kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) imeanza zoezi la kupanda miti katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma ikiwa ni sehemu ya kutunza mazingira.

Amesema shughuli ya upandaji miti imeenda sambamba na shughuli ya usafi wa mazingira, ambapo leo Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira kwa kushirikiana na wizara ya afya imefanya usafi katika eneo la soko la Mavunde (Soko la Chang’ombe) kama sehemu ya kuhamasisha wananchi kufanya usafi.

Naye Mwenyekiti wa Soko la Mavunde, Godfrey Mbilinyi ameishukuru Serikali kwa kuchagua kufanya usafi katika Soko hilo, kwani itaamsha hali kwa wafanyabiashara na wakazi wa Chang’ombe kufanya usafi na kupanda miti.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!