July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wizara Nishati yasikia kilo cha wachimbaji wadogo

Spread the love

WIZARA ya Nishati na Madini Tanzania inadhamiria kusaidia wachimbaji wadogo wa madini kwa kuwatengea hekali 197,432 na Dola za Marekan 3.4 milioni kama ruzuku. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo na msemaji wa wizara hiyo, Badra Masoud alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu juhudi za kuwaendeleza wachimbaji wadogo wa madini.

Badra amesema kuwa, hatua hiyo imekuja baada ya wachimbaji wadogo kuonekana kufanya kazi kwa kutumia dhana duni na katika mazingira magumu hivyo serikali imeamua kuwasaidia kwa kuwapatia fedha kama ruzuku na kuwatengea maeneo hayo kuweza kukuza kipato chao.

Amesema kuwa zoezila kutoa hekali kwa wachimbaji hao limezingatia kanuni namba 16 ya madini ya 2010 inayompa madaraka Waziri wa Ardhi kutenga maeneo kwa ajiri ya wachimbaji wa madini.

Masoud amesema kuwa kwa sasa maeneo 34 katika mikoa mbalimbali nchini, yametengwa kwa ajili hiyo ambayo ni pamoja na Mererani- Manyara, Kilindi-Tanga, Maganzo-Shinyanga, Winza-Dodoma, Ibaga-Singida, Nyakurungu-Mara, Vianzi-Pwani, na Sanza-Mbeya.

“Ruzuku hii ni jitihada za serikali za kutaka kuwakwamua wachimbaji wadogo wa madini kuondokana na umasikini ili waweze kufikia na kuwa wachimbaji wa kati,” amesema Masoud.

Pamoja na kuwapatia ruzuku wachimbaji hao, Masoud amesema serikali itaendelea kuwapatia pia elimu ya uchimbaji wa kisasa na namna ya kuepukana na ajali ndani ya migodi pia utunzaji wa mazingira katika maeneo wanayofanyia kazi.

“Iwapo mchimbaji au wachimbaji wa madini wadogo waliopewa mkopo hawatatumia fedha hizo walizopewaa kama walivyoomba Benki ya uwekezaji Tanzania (TIB) ambayo ndio imepewa dhama basi Benki hiyo itaweza kusitisha mkataba huu baada ya kushauriana na wizara ya nishati na madini,” amesema Masoud.

error: Content is protected !!