July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wizara: Jihadharini na kipindupindu

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Kebwe Steven Kebwe

Spread the love

WIZARA ya Afya na Ustawi  wa Jamii, imewahadharisha wananchi kujikinga na ugojwa wa mlipuko wa kipindupindu ulioingia kwa kasi nchini, kutokana na mwingiliano wa watu tofauti. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Inasemekana ugojwa huo umezuka ghafla mkoani Kigoma, kufuatia kuwepo kwa wimbi kubwa la wahamiaji tangu Aprili 26 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Naibu Waziri Afya, Dk. Kebwe Steven amesema mkoa wa Kigoma umepokea jumla ya wahamiaji 105,294, kutoka nchi jirani ya Burundi.

Amesema hadi sasa wagojwa walioripotiwa kuwa na dalili za ugojwa huo ni 2458.

“Wagonjwa wote hao walithibitika kutoka katika kambi maalumu ya wakimbizi ya Nyarugusu, iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma,” emesema Kebwe.

Amesema, watu wenye dalili za ugojwa huo wanazidi kuongezeka kila siku, ambapo hadi kufikia leo, wizara imepokea taarifa kutoka kwa Mganga Mkuu wa Kigoma kuwa, wagojwa wapya wapatao 588 wamepelekwa hospitali na waliofariki ni 15. 

Amesema kutokana na hali hiyo, wizara inatoa msisitizo kwa wananchi kuzingatia usafi, kwani kipindupindu ni ugonjwa hatari unaoambukizwa kwa kula chakula au kinywanji chenye vimelea vya “Vibrio cholera” ambavyo husababisha ugonjwa huo.

 “Vimelea hivi hupatikana kwenye kinyesi na matapishi ya mgonjwa wa kipindupindu au mtu mwenye vimelea ambaye hajaonesha dalili. Pia tunatoa angalizo kwa mikoa inayopakana na nchi ya Burundi,”amesema.

Kwa mujibu wa Kebwe, wizara kwa ushirikiano na Shirika la Afya Duniani (WHO), ilipeleka timu ya wataalam mkoani Kigoma kutembelea Kagunga, Nyarugusu, Lake Tanganyika Stadium.

Kwamba kwa kushirikiana na timu za afya za mkoa na wilaya pamoja na uongozi wa mashirika ya kimataifa yaliyoko Kigoma, wametathmini na kudhibiti hali hii ikiwemo kutoa elimu ya afya kwa umma na kupeleka dawa.

error: Content is protected !!