December 4, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wizara Afya yakabidhiwa hospitali ya Maweni

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dk.Zainab Chaula wakikabidhiana ripoti ya hospitali ya rufaa ya mkoa Maweni na Katibu Tawala wa mkoa wa Kigoma Rashid Machatta.

Spread the love

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekabidhiwa rasmi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Maweni. Anaripoti Mwandishi wetu, Kigoma…(endelea).

Akikabidhiwa hospitali hiyo, Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dk. Zainab Chaula amesema, anashukuru sekretarieti ya mkoa kwa kuisimamia hospitali hiyo pamoja na watumishi katika kipindi hicho na hivyo kuwezesha wananchi kupata huduma zinazostahili.

“Pamoja na makadhibiano, tutaendelea kushirikiana kwa ukaribu na ofisi yako RAS, na bado utaendelea kuwasimamia watumishi hawa kwani wapo mkoani kwako,” Dk. Zainab.

Aidha, Dk. Chaula amesema wizara yake imetengeneza mkataba kati ya Wizara na RAS katika eneo la usimamizi hasa ya majengo ili yaweze kubaki kwenye uimara unaohitajika.

“Tunawashukuru watendaji wa ofisi ya katibu tawala kwa kazi nzuri waliyoifanya ya usimamizi wa hospitali hiyo hadi sasa tunakabidhiana, tutakwenda kuzisoma nyaraka hizi moja baada ya nyingine, maana ni mali za Serikali, mmetueleza kuna madeni tutayapitia na kuyafanyia kazi,” alisema.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Rashid Machatta amesema, bado ataendelea kushirikiana kwa ukaribu na watumishi wa hospitali hiyo katika utekelezaji wa majukumu yao ili wananchi waweze kupata huduma bora

“ Watumishi sisi bado ni wamoja, tutashirikiana bega kwa bega ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma zilizo bora”.Alisema  Rashid Machatta.

Wakati huo huo Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dk. Osmond Dyegula amesema hospitali hiyo  ina jumla ya watumishi 233, kwa wastani wanaona wagonjwa kati ya 300 hadi 330 kwa siku kutokana na takwimu za mtuha za mwaka 2018/19.

Wizara ya afya imekabidhiwa hospitali hiyo ikiwa ni agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli kuhamishia usimamizi  huo wizara ya afya mwaka 2017  kutoka chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

error: Content is protected !!