TAASISI ya Elimu ya watu wazima (TEWW) imetoa wito kwa wananchi kujiunga na program za elimu ya watu wazima. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma (endelea).
Hayo yameelezwa leo Jumanne tarehe 25 Oktba, 2022 na Mkurugenzi wa taasisi hiyo Dk. Michael Ngumbi alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kwa malengo ya utekelezaji wa majukumu yao kwa mwaka wa fedha wa 2022/23.
Ngumbi amesema kuwa taasisi hiyo inatoa elimu kwa nadharia na vitendo Kwa kumjengea mwanafunzi uwezo wa kuwa mtu bora mwenye uwezo wa kujiendeleza na kupambana na changamoto za maisha.
Amesema taasisi imeongeza wigo wa kutoa elimu kulingana na uhitaji wa elimu ya watu wazima nchini na imekuwa na mchango chanya ambayo inamuwezesha mtu mzima kutatua changamoto za maisha katika mazingira anayoishi.
Aidha amesema kuwa jumla ya Billion 15 na million 531 zimetegwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 ikiwa ni Ongezeko la asilimia 7.2 ukilinganisha na bajeti ya mwaka 2021/2022 katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za taasisi ya Elimu ya watu wazima.
Taasisi ya elimu ya watu wazima ni taasisi ya umma iliyoanzishwa chini ya Wizara ya elimu , sayansi na teknolojia kwa lengo la kutoa na kusimamia elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi nchini.
Leave a comment