July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wito kwa wapenda michezo kufungua vyuo

Spread the love

WAZIRI Mkuu Kasimu Majaliwa ametoa wito kwa wadau na wapenda michezo kote nchini kufungua shule za michezo ili kuweza kuibua vipaji mbali mbali kwa manufaa ya taifa. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Wito huo ulitolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alipokuwa akifunga mbio za “Dodoma hapa kazi tu Half  Marathoni” zilizo fanyika mjini humo.

Amesema serikali ina nia ya dhati kuhakikisha inakuza sekta ya michezo yote hapa nchini kupitia Wizara husika.

Amesema umefika wakati wa kuanza kuibua vipaji vya watoto wadogo walioko mashuleni kwa manufaa ya kizazi cha leo na kijacho.

Waziri Mkuu alitumia wasaa huo kumwagiza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanii na Michezo, Nape Nnauye, kukutana na viongozi wa vyama vyote vya michezo kwa lengo la kusikiliza matatizo yao na kujua mahala mahala pa kuanzia.

“Serikali kupitia Wizara husika itakutana na vyama vyote vya michezo hapa nchini ili kila mmoja atueleze mipango yake kuanzia sasa na siku zijazo,” amesema Majaliwa.

Mbio hizo zilizotawaliwa na kauli mbiu “Dodoma hapa kazi tu Half Marathoni” zikiwa chini ya udhamini wa GSM Faundation,Kadco,NHC na Kilimanjaro Aloe Vera na TANAPA.

Amesema umefika wakati wa Tanzania kufanya vizuri na kufuta usemi kuwa Tanzania ni kichwa cha mwenda wazimu.

Katika mashindano hayo katika za mita 21 washindi watatu walipatiwa zawadi mbalimbali huku washindi 7wakipatiwa sh.50000 kila mmoja na mshindi wa kwanza akipatiwa zawadi ya pikipiki.

Kwa wanawake mshindi katika mita 21 mshindi wa kwanza Angelina Daniel toka Arusha amepata pikipiki,mshindi wa pili Fadhila Omari kota Arusha alipata bati 1000 huku mshindi wa tatu Asha Salum alipata bati 40.

Kwa upande wa ushindi wa wanaume km 21 Emmanuel Giniki amepata pikipiki,mshindi wa pili Gabriel Gerldi alipata mabati 100 na mshindi wa tatu Fabian Joseph alipata bati 40 wote kutoka Arusha.

error: Content is protected !!