Wednesday , 21 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wito kuhojiwa CCM; Makamba ‘nawasubiri’
Habari za SiasaTangulizi

Wito kuhojiwa CCM; Makamba ‘nawasubiri’

Spread the love

KOMREDI Yusuf Makama, Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ameonesha kutotikiswa na wito uliotolewa na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho, ili kumuhoji kwenye Kamati ya Usalama na Maadili. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole tarehe 13 Desemba 2019, Makamba na wenzake – Abdurahman Kinana (Katibu Mkuu Mstaafu CCM) na Bernard Membe (Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa) – wataitwa mbele ya kamati hiyo, kujibu tuhuma za kimaadili zinazowakabili.

Makamba na Kinana wanatuhumiwa kumdhalilisha mwenyekiti wa chama hicho, Dk. John Magufuli, ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Tanzania.

Akizungumza na chombo kimoja cha habari nchini, Makamba amekiri kuwa na taarifa za wito huo lakini hajapata barua rasmi.

Akijibu swali la mwandishi kuhusu kutekeleza wito huo ama la! Makamba amesema, waliotoa taarifa ya wito huo bado wapo Mwanza, na hivyo anawasuburi.

“…Suala lenyewe bado sana, hata waliosema haya wapo bado Mwanza, wakirudi, tukiitwa mtajua na hata tarehe mtaelezwa,” alisema Makamba na kuongeza;

“Nami nimesikia kama wewe,…lakini wito huwa haukataliwi, waswahili wana msemo usemao akuitae kajaza, ukichelewa atapunguza, hivyo sitachelewa ili asipunguze, nadhani jibu umelipata,” amesema Makamba.

Julai 2019, Kinana na Makamba walitoa waraka katika vyombo vya habari wakimtuhumu Cyprian Musiba, anayejipambanua kuwa mtetezi wa Rais Magufuli, kwamba anawachafua huku chama kikikaa kimya.

Waraka huo ulichafua hali ya hewa ndani ya CCM ambapo Mzee Makamba na Kinana, walianza kutuhumiwa kuwa na dhamira ya kumkwamisha Rais Magufuli katika juhudi zake za kulipeleka mbele taifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the loveSAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati...

error: Content is protected !!