May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Winga mpya Yanga: Mimi ni hatari kuliko Kisinda

Jesus Moloko

Spread the love

 

WINGA  mpya wa klabu ya Yanga raia wa Jamhuri ya Congo, Jesus Moloko amesema kuwa atawafurahisha mashabiki wa Yanga,  zaidi ya Tusila Kisinda ambaye ametimkia nchini Morocco, kwa kuwa yeye ni bora zaidi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezaji huyo ameingia kandarasi ya miaka miwili kuitumikia klabu ya Yanga, akitokea kwenye klabu ya AS Vita ya nchini Jamhuri ya Congo.

Moloko ambaye anakuja kuchukua nafasi ya Kisinda ndani ya kikosi cha Yanga, alisema kuwa anamfahamu mchezaji huyo kwa kuwa ni rafiki yake na wamecheza timu moja na atawafurahisha mashabiki wa yanga zaidi yake.

“Tusila ni rafiki yangu nimecheza naye timu moja na mimi ni mchezaji nitapambana na mashabiki mniamini na nitawafurahisha mashabiki kwa kuwa mimi ni bora kuliko Kisinda,” alisema.

Shaaban Djuma

Aidha mchezaji huyo aliongezea kuwa kila timu aliyocheza hajawahi kufeli na hivyo atapambana kuhakikisha timu hiyo inatwaa taji la Ligi Kuu.

Katika hatua nyingine klabu hiyo pia ilimtambulisha beki wa pembeni Shaaban Djuma kama mchezaji wao mpya akitokea kwenye klabu ya AS Vita ya nchini Congo.

Djuma ameingia mkataba wa miaka miwili na Yanga, ambao utamfanya kukaa kwenye klabu hiyo mwaka 2023.

Usajili wa wawili hao utafanya Yanga kutimiza idadi ya wachezaji nane waliowasajili mpaka sasa, kwenye msimu mpya ujao.

Wengine waliosajiliwa mpaka sasa ni David Brayson, Kharid Haucho, Dikson Ambundo, Djiugui Diarra, Fiston Mayele, Heritier Makambo na Yusuph Athuman.

error: Content is protected !!