Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko WiLDAF: Madawati ya jinsia yaanzishwe vyuoni kukali ngono
Habari Mchanganyiko

WiLDAF: Madawati ya jinsia yaanzishwe vyuoni kukali ngono

Mkurugenzi Mtendaji wa WiLDAF, Anna Kaluya
Spread the love

VYUO Vikuu nchini Tanzania, vimeshauri kuanzisha madawati ya jinsia ili kutokomeza vitendo hivyo vinavyojitokeza na kuathiri wanafunzi wawapo masomoni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumatatu tarehe 23 Novemba 2020 na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika (WiLDAF), Anna Kulaya wakati akitangaza kuanza siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia 25 Novemba – 10 Desemba 2020.

Anna amesema, katika kipindi hicho cha siku 16, watafanya shughuli kadhaa ikiwemo kupita vyuo mbalimbali nchini Tanzania kuzungumzia ukatili wa kijinsia na kuhamasisha uanzishwaji wa madawati ya jinsia.

“Kuwa na madawati ya jinsia kila vyuo, yatasaidia ili kama kuna mwanafunzi amefanyiwa ukatiri wa jinsia awe na sehemu ya kupeleka malalamiko yake,” amesema Anna.

Anna amesema, kumekuwa na ukatili mkubwa “sana vyuo vikuu na ripoti ya Takukuru inaonyesha asilimia 50 ya waliohojiwa wanasema kuna ukatili mkubwa vyuoni.”

Mkurugenzi huyo amesema, ukatili wa jinsia hususan kwa watoto na wanawake uko kila sehemu kuanzia ngazi ya familia, kazini na katika shughuli mbalimbali zinazohusisha mikusanyiko wa watu.

“Ni wakati wa kila mmoja sasa kwenye nafasi yake, kuwa sehemu ya mabadiliko katika kupinga na kutetea ukatili wa kijinsia. Tunahitaji kuutokomeza ukatili huu kama tutaamua,” amesema Anna

Amesema, kauli mbili ya mwaka huu ni; ‘Tuupinge ukatili wa kijinsia; Mabadiliko yanaanza na mimi.’

Anna amesema, ukatili umekuwa ukifanya pia kwa wanaume lakini wamekuwa wakiona aibu kujitokeza hadhani kuuzungumzia au kutoa ripoti katika madawati ya jinsia.

“Kila mtu achukue hatua kuhakikisha sauti za wahanga na wanaharakati zinasikika,” amesema Anna.

Kwa upande wake, Prudence Costantine, Msemaji wa wizara ya afya- Idara ya Maendeleo ya Jamii amesema, vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika kuuhabarisha umma juu ya masuala yanayohusu ukatili wa kijinsia.

Amesema, wiki ya Ukatili wa Kijinsia utakayoanza tarehe 25 Novemba 2020, itazinduliwa jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dk. John Jingu.

“Vitendo vya ukatili vimevuka mipaka na sasa kuna ukatili wa kisaikolojia kwa wanawake, watoto na hata wa baba wapo wanaofanyiwa vitendo hivyo,” amesema Costantine.

Vipigo, ubakaji, matusi na kunyimwa haki ya kumiliki ardhi na mengine mengi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

error: Content is protected !!