Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wilaya za Kagera, Kigoma kuunda mkoa wa Chato
Habari za Siasa

Wilaya za Kagera, Kigoma kuunda mkoa wa Chato

Spread the love

 

KAMATI ya Ushauri ya Mkoa wa Geita (RCC), imependekeza baadhi ya wilaya katika mikoa ya Kagera na Kigoma, zichukuliwe kwa ajili ya kuanzisha Mkoa mpya wa Chato. Anaripoti Mwandishi Wetu, Geita…(endelea).

Taarifa hiyo ilitolewa Ijumaa tarehe 29 Mei 2021 na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule, akitaja mapendekezo ya kikao cha kamati hiyo, kilichofanyika jana kwa ajili ya kujadili pendekezo la Wilaya ya Chato kuwa mkoa.

Senyamule alisema, kamati hiyo imependekeza baadhi ya maeneo katika Wilaya ya Kankonko mkoani Kigoma na Wilaya ya Biharamulo na Ngara za mkoani Kagera, zitumike kuunda mkoa huo.

“Mkoa wa Chato imependekezwa kutoka katika Mkoa wa Geita na iwe na Wilaya ya Chato yenyewe na Bukombe, lakini pia tumependeka kutoka Kigoma tuombe baadhi ya eneo kutoka Wilaya ya Kakonko na kutoka Mkoa wa Kagera tuombe wilaya mbili ya Biharamulo na Ngara, ambazo kwa pamoja zitaunda Mkoa wa Chato,” alisema Senyamule.

Senyamule alisema, mapendekezo hayo yatapelekwa katika wizara husika, kwa ajili ya kufanyiwa kazi.

“Mapendekezo haya yamekamilika na kukubaliwa na wajumbe wote, sasa yaptapelekwa kwenye wizara husika ili yafanyiwe kazi,” alisema Senyamule.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Geita, alisema kama mapendekezo hayo yatakubalika serikalini, Mkoa wa Geita utabaki na wilaya zake tatu, pamoja na wilaya ya Sengerema, kama mapendekezo ya kamati hiyo ya kuitoa wilaya hiyo kutoka mkoani Mwanza, yatakubaliwa.

“Kikao cha RCC kilichokaa kama kikao maalumu kwa ajili ya mapendekezo ya kuunda Mkoa mpya wa Chato, kimependekeza yafuatayo, kimependekeza mkoa mama wa Geita ibakie na wilaya tatu ambazo ni Geita yenyewe, Mbogwe na Nyang’wale, ambazo tayari zipo,” amesema Senyamule.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Geita aliongeza “RCC pia inapendekeza iombwe Wilaya ya Sengerema ambayo iko Mkoa wa Mwanza, ili iweze kukamilisha idadi ya wilaya nne, pamoja na Wilaya pendekezwa ya Busanda.”

Pendekezo la Chato kuwa mkoa lilitolewa tarehe 26 Machi 2021, na Mzee wa Wilaya ya Chato, Samwel Bigambo, mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan, katika mazishi ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania, Hayati John Magufuli.

Bigambo alimuomba Rais Samia aifanye Chato kuwa mkoa, ili kumuenzi Magufuli, aliyefariki dunia akiwa madarakani, tarehe 17 Machi 2021, kwa ugonjwa wa moyo, kwenye Hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam.

Magufuli aliyezikwa kijijini kwao Chato mkoani Geita, aliiongoza Tanzania kwa miaka mitano na miezi mitano mfululizo (Novemba 2015-Machi 2021), hadi umauti ulipomkuta akiwa katika muhula wake wa mwisho, wa uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano, uliokuwa unafika tamati 2025.

Kufuatia kifo cha Magufuli, Samia aliyekuwa Makamu wake wa Rais, aliapishwa tarehe 19 Machi 2021, katika Ikulu ya jijini Dar es Salaam, kurithi mikoba yake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!