Thursday , 7 December 2023
Home Kitengo Michezo Wikiendi ngumu: Kule Simba SC, huku Yanga
MichezoTangulizi

Wikiendi ngumu: Kule Simba SC, huku Yanga

Spread the love

TOFAUTI na misimu iliyopita, msimu huu 2019/20 mambo yamechenji kidogo. Simba na Yanga zinatarajiwa kufungua msimu huu kwenye michuano ya kimataifa Jumamosi wiki hii, badala ya kuanza kucheza Ligi Kuu kama ilivyozoeleka. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Yanga kesho tarehe 10, Agosti 2019, atajitupa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam kumenyana na Township Rollers ya Botswana katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Marudiano ya mchezo huo yatafanyika mjini Gaborone, Botswana kati ya Agosti 23 na 25, mwaka huu.

Tofauti na mechi za awali ambazo tayari imecheza, kwenye mchezo huo Yanga italazimika kukaza msuli ili kuendeleza hamasa iliyonayo mashabiki wake kwa sasa.

Katika kuhakikisha Yanga inapata matokeo chanya kwenye mchezo huo wa kwanza, kikosi hicho kinachonolewa na Kocha wake Mkuu, Mwinyi Zahera, Yanga imejichimbia Visiwani Zanzibar.

Yanga inavaana na Township Rollers ikitokea kambini Visiwani Zanzibar, na kucheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Mlandege na Malindi FC, kabla ya hapo walicheza na Kariobangi Sharks ya Kenya mcheo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Wakiwa Zanzibar, mchezo wake wa kwanza, Yanga iliitandika Mlandege mabao 4-1, lakini mchezo wake wa pili uliochezwa jana tarehe 8 Agosti 2019, ilitoka sare ya 1-1 dhidi ya Malindi FC.

Kocha Zahera amejigamba kwamba, Yanga ipo imara kiasi cha kumchanganya na kushindwa kupanga kikosi cha kwanza kutokana na wachezi wake wote kuwa imara.

“Kikosi kinaendelea kufanya vizuri, kila mchezaji hapa anajituma sana na kutoa alichonacho kwa ajili ya timu,” alisema Kocha Zahera baada ya mchezo wake na Malindi na kuongeza: “Mpaka pale nitakaporudi Dar es Salaam, nitakuwa tayari nimejua nani anapaswa kuanza na nani atafuata.”

Simba na mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2017/18 na 2018/19 wanakwenda kuikabilia UD Songo ya nchini Msumbiji. Mechi hiyo inachezwa kesho tarehe 10 Agosti, 2019 kwenye mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Patrick Aussems, Kocha Mkuu wa Simba ametamba kwamba ‘Simba hii haina utani’ na kwamba, atamaliza kazi mapema.

Kama ilivyo kwa Yanga, Simba nao watarudiana na UD Songo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kati ya Agosti 23, 24 na 25 mwaka huu.

Kocha Aussems anasema, kikosi chake kimeiva, kimefanya maandalizi mazuri na kwamba kina kila sababu ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo wa kwanza.

Hata hivyo ameeleza kuwa, Ibrahim Ajib, Aishi Manula na Wilker Henrique hawajawa fiti kuanza kwenye kikosi hicho kutokana na majeraha waliyonayo.

Simba awali ilikwenda kunoa silaha zake nchini Afrika Kusini kwa wiki mbili huku ikijiandaa kuelekeza nguvu kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara kwa lengo la kuchukua taji kwa mara ya tatu mfululizo.

Katika michuano ya kimataifa, Simba ilionekana kufanya vema hasa kwenye mechi zake zote za nyumbani, ilicheza bila kupoteza hata mechi moja nyumbani. Ilipenya na kwenda hadi robo fainali katika michuano hiyo. Ndoto ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo ilikatishwa na TP Mazembe kutoka DR Congo.

Je, Simba inaweza kufanya maajabu kama msimu uliopita? Yanga inaweza kuvunja rekodi ya Simba msimu uliopita katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika? Je nani anaanza kwa matumaini hiyo kesho? Tusubiri, tuone.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Piga mkwanja wa kutosha katika usiku wa kibabe kati ya Man United vs Chelsea

Spread the love USIKU wa leo katika dimba la Old Trafford utapigwa mchezowa...

BiasharaTangulizi

Bei ya Dizeli, Petroli yashuka

Spread the loveBEI ya mafuta kwa mwezi Disemba, imeshuka kutokana na kupungua...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

BiasharaMichezo

Mwana FA anogesha Tamasha la Exim Bima Festival

Spread the loveNAIBU Waziri Wa Utamaduni, Sanaa Na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘Mwana...

error: Content is protected !!