Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari Wiki ya uchanjaji yaja, bilioni 83 kujenga kiwanda cha chanjo
Habari

Wiki ya uchanjaji yaja, bilioni 83 kujenga kiwanda cha chanjo

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania imesema, wiki ya mwisho wa mwezi Septemba au mwanzo wa Oktoba 2021, itaanzisha wiki ya uchanjaji chanjo ya virusi vya corona (COVID-19). Anaripoti Gabriel Mushi (endelea…).

Akizungumza na waandishi habari pamoja na Watanzania leo tarehe 12 Septemba jijini Dodoma, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema katika wiki hiyo viongozi mbalimbali wa serikali watashiriki ili kuhakikisha wananchi wa maeneo ya vijijini wanapata chanjo.

Amesema hadi kufikia Septemba 2021, asilimia 34 ya chanjo zilizoingizwa nchini sawa na Watanzania 345,000 wamechanja chanjo ya corona.

Msigwa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo amesema, ili kufikia wengi zaidi pia serikali italeta chanjo nyingine ikiwamo za aina tofauti na Johnson&Johnson.

Pia, amesema Serikali inatarajia kutumia kiasi cha Sh.83 bilioni kujenga kiwanda cha chanjo ya corona na nyingine za binadamu.

Gerson Msigwa, Msemaji wa Serikali

“Fedha hizo ni kati ya Sh.1.3 trilioni ambazo tayari zimeidhinishwa na Shirika la Fedha Duniani (IFM) kuisaidia maeneo ya Tanzania yaliyopata madhara kutokana na Corona.”

“Muda wowote kuanzia sasa Serikali itapokea kiasi cha Sh.1.3 trilioni kutoka Shirika la Fedha Duniani (IFM) kwa ajili ya kusaidia maeneo yaliyopata madhara kutokana na maambukizi ya Corona. Maeneo hayo ni sekta ya utalii, huduma za kijamii kama vile maji na elimu,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!