Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Wiki hii kwa ufupi…
Habari Mchanganyiko

Wiki hii kwa ufupi…

Spread the love

Mbatia: Nani mwenye kiburi?

MWENYEKITI wa NCCR- Mageuzi, James Francis Mbatia (55), ameonya kuwa hakuna maendeleo yanayoweza kufikiwa nchini, ikiwa umoja wa kitaifa uliosisiwa na Mwalimu Julius Nyerere, utavurugwa na warithini wake. Anaandika Mwandishi Wetu…(endelea).

Akizungumza kwenye mkutano mkuu wa chama chake, tarehe 27 Julai kwenye ukumbi wa Diamond Jublee, Mbatia amesema, ili taifa liwe na maendeleo, lazima serikali na wananchi wake waondokane na ubinafsi.

Amesema, “…imani zote zinatufundisha udugu, utu na umoja; sasa ni nani mwenye kiburi?  Yatubidi kujitafakari upya,  kujitambua na kujua misingi ya taifa yetu.”

JPM aumiza kichwa

RAIS John Magufuli, ameibua maswali yanayomuumiza kichwa kuhusu tukio la kukamatwa kwa dhahabu ya Tanzania nchini Kenya, bila watuhumiwa kukamatwa.

Amehoji, inawezekanaje dhahabu ikapenye kwenye mipaka ya Tanzania, nchi yenye vyombo vya usalama na kisha ikakamatwe na vyombo vya usalama nchini Kenya?

Dhahabu ya Tanzania kiasi cha kilogram 35.34, ilikamatwa na vyombo vya usalama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta nchini Kenya mwaka 2018, leo tarehe 24 Julai 2019 imekabidhiwa kwa Rais Magufuli.

JPM aagiza mabadiliko ya haraka TAZARA

RAIS John Magufuli ameagiza mchakato wa urekebishaji Sheria ya Reli inayounganisha nchi za Tanzania na Zambia (TAZARA), kufanyika haraka ili kuboresha shughuli za usafirishaji wa abiria na mizigo.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo tarehe 25 Julai 2019 akiwa safarini kuelekea Kisaki mkoani Morogoro kwa kutumia usafiri wa treni.

Pia amewaagiza viongozi wa TAZARA kuwasilisha mapendekezo yao juu ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kuboresha usafirishaji wa mizigo na abiria kupitia TAZARA.

Kesi ya Mbowe: Mahakama yakubali ushahidi wa Jamhuri

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai 2019, ilipokea kielelezo cha kamera ya kurekodi video na tepu vilivyowasilishwa na Jamhuri.

Kielelezo hicho kilichopingwa mahakamani hapo na upande wa utetezi, katika kesi inayowakabili viongozi waandamizi wa Chadema.

Viongozi wa chama hicho wanatuhumiwa kufanya uchochezi. Viongozi hao ni Freeman Mbowe, mwenyekiti Taifa; Dk.Vicent Mashinji, Katibu Mkuu: John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu-Bara na Salumu Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu-Z’Bar.

Wengine ni Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini; Halima Mdee, Mwenyekiti wa Bawacha-Taifa; Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini; John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini na Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini.

CCM washughulikiana Hanang’

KAMATI ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilayani Hanang’ katika Mkoa wa Manyara imefuta uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Viajana (UVCCM), wilayani humo kwa madai ya kugubikwa na rushwa.
Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Hanang’ Mathew Dareda alisema uchaguzi huo uliokuwa ufanyike Jumamosi, iliyopita umefutwa na kamati ya siasa ya wilaya hiyo.

Uchaguzi huo mdogo ulipangwa kufanyika ili kuziba nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM wa Wilaya, Ester Mchome, ambaye ameajiriwa serikalini na Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, kuwa Ofisa Mtendaji Kata ya Bargish.

Dengue yaua 13

UMMY Mwalimu, Waziri wa Afya, Maenfdeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, amesema watu waliofariki dunia kwa homa ya dengue ni 13 huku waliougua ugonjwa huo wakiwa 6,677.

Mwalimu alisema hayo wakati akizindua wa mkakati wa kupambana na mbu na wadudu wengine, shughuli iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na kuwa awali, takwimu zilionyesha vifo vilikuwa sita lakini serikali ilifanya tathmini upya na kupata takwimu sahihi.

Uzembe, mwendokasi wauwa 34

ASKARI Polisi watatu walifariki dunia na wawili kujeruhiwa katika ajali iliyotokea kwenye Kijiji cha Kilimahewa, Barabara ya Kilwa Wilaya ya Mkuranga, Mkoa wa Kipolisi Rufiji.

Msemaji wa Polisi Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), David Misime, alisema askari hao waliokuwa kwenye gari lenye namba za usajili PT.3822 aina ya Toyota Cruiser mali ya jeshi hilo ambapo walikuwa wakitokea Ikwiriri kwenda Kijiji Cha Mwalusembe.

Alisema gari hilo lilipasuka gurudumu la nyuma upande wa kulia na kupinduka na kusabababisha vifo vya askari vifo na majeruhi.

Stigler’s Gorge kukamilika 2022

RAIS John Magufuli tarehe 26 Julai 2019 amezindua ujenzi wa Mradi wa Uzalishaji Umeme katika Mto Rufiji (Stigler’s Gorge), unaogharimu kiasi cha Sh. 6.5 trilioni.

Mradi huo unatarajiwa kukamilika tarehe 13 Julai 2022. Ameshauri askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kushiriki katika ujenzi huo, ili wapate ujuzi watakaoutumia katika ujenzi wa miradi mingine.

Pia ameagiza mamlaka husika kushughulikia haraka vibali vya wafanyakazi wa kigeni, ili ujenzi huo uanze haraka. Pia ameagiza Wizara ya Nishati kuhakikisha kwamba mradi huo unatumia bima ya serikali kwa asilimia 100.

 ‘Upigaji’ wa kutisha Selou

Rais John Magufuli ameeleza kuwepo kwa wasiwasi wa kuporwa mabilioni ya fedha, kunakofanywa na maofisa wa pori la akiba la Selous huku akitilia shaka kama serikali inaambulia chochote. 
Rais Magufuli aliyasema hayo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa bwawa la mradi wa kufua umeme kwenye Mto Rufiji (Stiegler’s George) unaotarajiwa kugharamu Sh. trilioni 6.5 kwa lengo la kuzalisha MW 2,115.>
Hata hivyo alisema, mradi huo kwa muda mrefu umeshindwa kutekelezwa kutoka na kupigwa vita kutoka ndani na nje ya nchi, ili serikali iendelee kuuziwa umeme kwa gharama kubwa

Bashe, Simbachawene wateuliwa

SIKU mbili kupita baada ya Hussein Bashe, Mbunge wa Nzega Mjini kuwakaripia Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba, kutokana na barua yao waliyoiandika wakilalamikia kudhalilishwa na mwanaharakati anayejitambulisha kuwa mtetezi wa Rais John Magufuli-Cryspian Musiba, aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.

Bashe aliwatuhumu wazee hao waliovuja jasho kumvusha Rais Magufuli kwenye uchaguzi mkuu uliopita kwamba, wanataka kukivuruga chama.

Lissu mgonjwa: Mahakama yaridhia

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imeahirisha kesi ya uchochezi inayowakabili wahariri wa Gazeti la Mawio, kutokana na mshitakiwa wa nne (Tundu Lissu), kuwa mgonjwa. 

Mshitakiwa wa kwanza kwenye kesi hiyo ni Jabir Idrisa, mwandishi mwandamizi wa gazeti hilo, mshitakiwa wa pili ni Simon Mkina, Mhariri, Ismail Mahboob, Meneja wa Kampuni ya uchaishaji ya Flint na mshitakiwa wa nne ni Tundu Lissu, aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki.

Zitto toa rai kwa viongozi wa dini

ZITTO Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo ametoa wito kwa viongozi wa dini kukemea vitendo vya baadhi ya viongozi wa siasa, wanaohatarisha amani ya nchi.

Zitto ametoa wito huo tarehe 27 Julai 2019 katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la EAGT, lililoko Yombo Kilakala Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Mteule wa JPM atuhumiwa kuomba rushwa

MTEULE wa Rais John Magufuli, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Hai (DC), Ole Sabaya  anatuhumiwa kumwomba rushwa mfanyabiashara Curthebert Swai wa jijini Arusha.

Swai ambaye ni mmiliki wa Hoteli ya Kitalii ya Weruweru River Lodge, alirekodi kipande cha video akieleza namna Sabaya alivyomwomba rushwa ya Sh. 5 milion.

Hata hivy, Sabaya alijibu kuwa uamuzi wa Swai kudai kuombwa rushwa, unatokana na yeye (Sabaya) kumwondoa Swai katika eneo alilompora bibi mjane Mary Diriwa (86).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Soko nepi za watoto lashuka, watu wazima lapaa

Spread the loveKiwanda cha kutengeneza nepi cha Japan kimetangaza kuwa kitaacha kutengeneza...

error: Content is protected !!