Wednesday , 24 April 2024
Home Kitengo Michezo Wikendi  yawa mbaya kwa vigogo wa soka barani Ulaya
Michezo

Wikendi  yawa mbaya kwa vigogo wa soka barani Ulaya

Spread the love

 

Baadhi ya vigogo vya soka Barani Ulaya vimekua na wikendi mbaya baada ya kupoteza michezo yao ya ligi kuu na kupoteza alama tatu muhimu .Anaripoti Damas Ndelema TUDARCo(endelea)

Wikendi ilianza kua mbaya siku ya jumamosi kwa klabu ya Barcelona ambao wamekua na mwendelezo mbaya wa matokeo klabu hiyo inayoshika nafasi ya tisa ilikubali kichapo cha mabao 2-0 ugenini dhidi ya klabu ya Atletico Madridi  na kufanya hali kuzidi kua mbaya kwa klabu hiyo ambayo ilitoka kupoteza mchezo katikati ya wiki katika ligi ya Mabigwa barani Ulaya dhidi ya Benifca Fc kwa bao 3-0.

Huku siku ya jana vigogo wengine wa nchini Hispania klabu ya Real Madrid nao walikubali kuacha alama tatu muhimu baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 ugenini dhidi ya klabu ya Espanyol na kufanya madrid kusalia nafasi ya kwanza na pointi zao saba baada kushuka dimbani mara nane

Aidha wikendi iliendelea kua mbaya kwa siku ya jana baada ya kushudia vigogo wa Ufaransa,  klabu ya PSG kukubali kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya klabu ya Rennes na kuondoa utawala wa PSG ambao walikua wamecheza mechi nane za ligi kuu bila kupoteza .

Pia kigogo wa ligi kuu Ujerumani Bayern Munich  jana walikubali kichapo cha mabao 1-2 nyumbani dhidi ya klabu ya Eintracht Frankfurt, nao mashetani wekundu Manchester United wameshindwa kuwa na mwendelezo mzuri wa matokeo baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 nyumbani dhidi ya klabu ya Everton na kufanya vigogo hao kushika nafasi ya nne wakiwa na pointi zao 14 baada ya kushuka dimbani mara saba

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

Michezo

Ujanja ni kubeti na Meridianbet

Spread the love  JUMAPILI ya leo imekaa kihela hela sana ndani ya...

Michezo

Anza Jumamosi yako na mkwanja wa Meridianbet

Spread the loveJumamosi ya leo ODDS zimekaa kijanja sana ndani ya Meridianbet...

error: Content is protected !!