
Zao la Tumbaku
SHIRIKA la Afya Duniani (WHO), limezitaka serikali duniani kuongeza kodi za bidhaa za tumbaku kwa kuwa huenda vifo vikaongezeka na kufikia milioni nane kwa mwaka ifikapo mwaka 2030 kama hatua zaidi hazitachukuliwa dhidi ya uvutaji sigara.
Uvutaji tumbaku unachangia vifo vya watu milioni sita kila mwaka kote duniani hivi sasa hii ikiwa idadi kubwa kuliko vifo vinavyosababishwa na ugonjwa Malaria, Kifua Kikuu na Ukimwi .
Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Margaret Chan amesema kuongeza kodi ya bidhaa za tumbaku ni mojawapo ya njia bora za kupunguza uvutaji wa sigara ambazo zinawaua mamilioni ya watu.
Source BBC Swahili.
More Stories
Waziri Ummy azindua mitambo ya hewa tiba ya oksijeni yenye thamani ya bilioni 1.5
Mapacha walioungana vifua watenganishwa Muhimbili
NMB yakamilisha ujenzi wa zahanati iliyokwama miaka 10 Pwani