October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

WHO yaidhinisha chanjo ya kwanza ya Malaria, ilisakwa kwa miaka 100

Spread the love

 

SHIRIKA la Afya duniani (WHO) limeidhinisha chanjo ya kwanza ya ugonjwa wa Malaria na kusisitiza kuwa inapaswa kutolewa kwa watoto wote Barani Afrika, ili kuchochea juhudi za kuzuia kuenea kwa maradhi hayo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumzia mafanikio hayo, Mkurugenzi wa WHO, Tedros Ghebreyesus ameitaja hatua hiyo kuwa ya kihistoria.

Amesema uamuzi huo unatokana na matokeo ya utafiti unaoendelea katika nchi za Ghana, Kenya na Malawi uliowafuatilia watoto zaidi ya 800,000 waliopatiwa chanjo ya Malaria tangu mwaka 2019.

Mkuu wa WHO, Dk. Tedros Adhanom Ghebreyesus

Chanjo hiyo – inayoitwa RTS, S – ilithibitishwa kuwa na ufanisi miaka sita iliyopita.

Pia ilitengenezwa na kampuni ya madawa ya Uingereza ya GlaxoSmithKline mwaka 1987 na ina ufanisi wa asilimia 30.

Aidha, majaribio ya kuitafuta chanjo hiyo, yamefanyika kwa miaka 30 licha ya kwamba kuna makampuni mengine yalianza kwa zaidi ya miaka 100.

error: Content is protected !!